The New Stuff
LIFAHAMU KUNDI LA RAU UNIT
RAU UNIT
Hili
ni kundi la muziki wa HIPHOP lililoanzishwa na wasanii wa muziki huo
kutoka mtaa wa Rau, Moshi mjini.Kundi hili linajumla ya wasanii watatu
Bambino,Baraka na Roger chini ya mwamvuli wa mtaa wa Rau.
CHIMBUKO LA RAU UNIT:
Chimbuko la kundi
ni msanii Bambino ambaye ndiye aliyekuja na wazo la kuanzisha kundi la
mziki wa Hiphop RAU mwanzoni kundi lilitambulika kama MASHUJAA il baadae
lilibadili jina na kuitwa RAU UNIT ikiwa ni lengo la
kuitanua Hiphop Rau na kuimiza umoja kwa wasanii wa Hiphop Rau na Moshi
kwa ujumla.
KAZI ZINAZOFANYWA NA KUNDI:
Kundi la RAU UNIT linafanya kazi mbalimbali za muziki kazi hizo ni kama zifuatazvyo;
Kundi linafanya Rapping au mziki wa kufokafoka
Kundi linaandika mashairi ya nyimbo mbalimbali mf. Hiphop,Rnb
Kundi linafundisha uandishi wa mashairi
Kundi linafanya tafiti mbalimbali za kimuziki Tanzania
MTAZAMO AU MALENGO YA KUNDI;
Kundi lina mtazamo nwa kimapinduzi katika sanaa ya Tanzania.
Kundi lina malengo ya kuinua mziki wa Hiphop Moshi kwa kupitia kazi mbali mbali linazofanya.
VIKWAZO AU CHANGAMOTO;
Kundi linakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosekana kwa ushirikiano kutoka kwa wasanii wengine wanaofanya muziki
Vilevile kundi linakabiliwa na kuwepo
kwa imani potofu miongoni mwa wanajamii juu ya muziki wa Kizazi kipya
kuwa ni muziki wa kihuni
AZIMIO:
Kundi limeazimia kukabiliana na vikwazo na changamoto zote zinalolikabili kwa kufanya harakati mbalimbali za kimuziki.
HITIMISHO:
Kundi linatoa pongezi kwa wadau wote
wa muziki Tanzania kwa kuimarisha muziki nchini hususa muziki wa kizazi
kipya pia kundi linatoa pongezi kwa wasanii mbalimbali wa HIPHOP
Tanzania kwa kuisimamisha nguzo hiyo muhimu hapa nchini MUNGU IBARIKI
TANZANIA MUNGU IBARIKI SANAA.
0 comments:
Post a Comment