background img

The New Stuff

_RAP INFINITY ISIKILIZE HAPA NGOMA KALI KUTOKA KWA JIMMY ROCK

Ashura aliiona siku yake kuwa ya kipekee sana mchana wa siku ile, alitamani siku kama ile ingewai kufika kwani alikuwa akiisubiri na kuitamani kila asubuhi aliyokuwa mbele ya dressing table kubwa chumbani kwake, hatimaye ilifika siku aliyoiota kila usiku na kutamani iwe ndoto ya kweli. Muda wote Ashura alionekana mchangamfu isivyo kawaida yake
‘Eh! Shosti kulikoni mbona unatabasamu mwenyewe na hyo simu?’ aliuliza Anitha rafiki wa Ashura ambaye pia walikuwa wakifanya kazi ofisi moja
‘Its just nothing mamy’ alijibu Ashura kwa sauti ya kudeka huku akimgeukia Anitha aliyekuwa akimtazama kwa mshangao

Saa kumi jioni ndio muda wa Ashura kutoka ofisini muda ambao siku zote aliuona kama ni mapema sana kwake kwenda nyumbani lakini leo aliuona kama ni muda uliochelewa sana kufika, hamu yake yote ilikuwa ni kuwasiliana na ata kuonana na Abuye kijana aliyekutana nae masaa machache yaliyopita na kubadili kabisa mtazamo wa binti huyu. Hatimaye saa kumi ilifika Ashura haraka haraka alizima computer kubwa iliyokuwa mbele yake huku akijisogeza ndani ya kiti cha kuzunguka kilichiuwa a nakshi maridhawa za rangi ya silva

‘mamy see you, I have something very important today’ aliaga Ashura huku akijiweka sawa tayari kuelekea alipo park gari tayari kuanza safari ya kurudi nyumbani
‘its everything fine!?’ aliuliza Anitha huku akiwa na mshangao kidogo kwani haikuwa kawaida ya Ashura kuwahi kutoka kazini tena akiwa katika hali isiyoeleweka
‘yeah mamy, ok bye!’ alijibu Ashura huku akionekana kutokutaka maongezi mengi

Akiwa ndani ya gari Ashura alimpigia Abuye simu namba ikawa inatumika, alisononeka kidogo lakini akajipa moyo akifika nyumbani atamtafuta tena. Njiani Ashura alikuwa ni mtu mwenye furaha ya ghafla ambayo hata yeye mwenyewe alijihisi kuwa hayupo kawaida ila kwa vile aliijua sababu hata hakuangaika kuumiza kichwa kuifikiri ilipotoka furaha yake. Baada ya nusu saa Ashura alikuwa tayari amefia nyumbani mawazo na akili yake yote yalikuwa kwa Abuye hakutaka kupotea kabisa muda alifanya mambo yote yanayotakiwa kufanywa na mwanamke kasha akajipumzisha juu ya kitanda kikubwa cha sita kwa sita.

Ashura alichukua simu na kumpigia Abuye, baada ya sekunde chache sauti ya kiume iliyosema ‘Allo!’ ilipenya kwenye sikio la Ashura, kimya kikapita bila kujua ajibu nini kasha kwa uoga Ashura alijibu salamu na kumjulia hali Abuye
‘Alo!, mambo vipi mwaya’ kwa sauti nyembamba ya upole aliuliza Ashura
‘Poa, sista mambo?’ alijibu Abuye kwa kujiamini
‘safi tu wangu, unapenda kuniita sista ee!’ alijibu na kuchomekea swali Ashura
‘kawaida tu sista angu, nimeshazowea kutumia jina ilo kwa watoto wa kike’ aliendelea Abuye
‘haha! Eti watoto wakike, haya basi mimi nataka uchague jina la kuniita mimi, ila tofauti na hili’ alijichekesha Ashura huku akijishaua kitandani kwake
‘ah!, poa nitakutafutia kwanzia kesho nitakubadilishia jina’ aliongezea Abuye ‘ungependa nikuite jina gani ulipendalo?’
‘Aaa! Mimi lolote tu zuri utakalochagua wewe’

Waliendelea na maongezi ya hapa na pale kuweza kufahamiana zaidi kadiri maongezi yalivyozidi ndivyo na furaha ya Ashura ilizidi kuongezeka, Ashura alimsimulia Abuye histora yake japo kwa ufupi, huu Ashura naye akiiskiliza historia ya Abuye ndipo aligundua kuwa Abuye alikuwa ni mwanafunzi katika moja ya vyuo jijini Dar es Salaam akisoma shahada ya sheria. Ashura alizidi kuvutiwa zaidi na Abuye aliyeonekana na uwezo mkubwa wa kuongea na kujiamini. ‘hakika huyu ndiye mwanaume anayenifaa’ aliwaza Ashura wakati akimsikiliza Abuye. Baada ya maongezi ya takribani saa nzima Abuye alimwambia Ashura kuwa anaitaji kupumzika kidogo kwani amechoka sana na pilika pilika za siku nzima

‘Ah! Mbona mapema sana jamani, vipi umekula kweli hata?’ aliuliza Ashura kwa unyonge kwani stori zilikuwa zimeshamkolea
‘Nimechoka tu Ashura, nitakula nikiamka mida ya saa mbili’ alisema Abuye huku akijua wazi kuwa Ashura asingependa amuache peke yake
‘sawa’ alijibu Ashura kwa unyonge ‘ukiamka uni text mwaya’
‘Ok usijali nikiamka tu utakuwa mtu wangu wa kwanza kuwasiliana naye Ashura’ alijibu Abuye kwa uchangamfu jibu lililompa matumaini Ashura
‘Ok baadae, sleep tight’ alijibu Ashura.

Baada ya kujibu na kukata simu ilikuwa tayari ni mida ya saa 12 na dakika saba, Abuye alijilaza kwa uchovu haikupita muda mrefu akawa tayari ameshachukuliwa na usingizi.

Kwa Ashura saa 12 ulikuwa ni muda wa kuangalia habari mbali mbali za kimataifa BBC News Channel, ila kwa siku ile aliamua kujishuhulisha na shuhuli ambazo angezifanya saa mbili usiku ili apate uda mzuri wa kuongea na Abuye, taratibu ratiba yake ya kila siku ilianza kubadilika japo aliona kama jambo la kawaida tu!, muda wote aliokuwa akijishuhulisha alimuwaza Abuye, aliiwaza sauti yake akauwaza mwili wake uliokuwa si mfupi wala si mrefu sana unaweza kuuita mwili wa kati si mnene sana wala si mwembamba pia, Ashura alizidi kutamani siku moja auguse japo mara moja tu!. ‘Ah! Kajialiwa sauti sawa na mwili wake, jamani duniani kuna wanaume ma handsome adi wa sauti’ aliwaza Ashura huku akitabasamu

Inaendelea... 

Ah! NIONGEZEE (2)

DOWNLOAD HAPA! HUU MZIKI

MJUE ZAIDI:

Anaitwa Melissa michael kwa upande wa sanaa anajulikana kama Michy . Ni mwanafunzi wa sheria UDSM mwaka wa kwanza . Upcoming artist ambaye alituma demo yake katika studio za de fatality kilichopelekea kuonekana ana mwanga mzuri wa mziki na kupewa ofa ya kurekodi nyimbo yake mpya inayotambulika kama HUU MZIKI . Video ipo tayari chini ya utayarishaji wa director @Hanscana_  huku audio production ikisimamiwa na producer @mesenselektatz 

SIKILIZA NA DOWNLOAD HAPA HUU MZIKI YA MICHY STAA MPYA KUTOKA DE FATALITY

Popular Posts