Hip hop ni aina ya muziki unaoelezea aina ya usanii na utamaduni fulani uliyotokana na jamii ya Wamarekani Weusi na Walatino kunako miaka ya 1970 huko mjini New York City, hasa katika kitongoji cha Bronx.The Bronx ni moja kati ya sehemu za New York City, Marekani. Jina linatokana na Bronck's Farms, ambalo linamilikiwa na mlowezi mmoja aitwaye Jonas Bronck. DJ Afrika Bambaataa alieleza kwa muhtasari wa nguzo nne za utamaduni wa hip hop: U-MC, U-DJ, breaking na uandikaji wa graffiti.
Graffiti ni alama au maandishi yaliyochorwa katika ukuta. Kikawaida hufanywa na rangi au kidude cha kupulizia rangi (rangi inayopulizwa kutoka katika kikopo). Alama moja yaweza kuitwa graffito lakini neno graffiti kikawaida hutumika kwa maana ya kwamba kuna alama zaidi ya moja.
Graffiti inaweza kuchukua umbo la sanaa, michoro au maneno. Hatua hii ikifanyika bila ya idhini ya mwenye mali huhesabiwa kama uhuni. Wakati mwingine watu huchora na kuandika jina la mtu au maneno makali(matusi). Wakati mwingine huwa kama upingaji wa umma kisiasa.
Elementi zingine ni pamoja na beatboxing.
Beatboxing ni jina la kutaja aina ya upigaji ngoma kwa kutumia mdomo - hasa kwa kuhusisha sanaa ya utayarishaji wa midundo ya ngoma, wizani,
na sauti za kimuziki kwa kutumia mdomo wa mtu, midomo, ulimi, na sauti.
Pia inaweza kuhusisha kuimba, sauti za mwigo wa hali ya turntable, na
pia uigaji wa honi, nyuzi za gitaa, na vyombo vingine vya muziki. Leo
hii beatboxing inahusiana na utamaduni wa hip-hop, ikiwa kama moja kati ya "elementi" zake, ijapokuwa mwisho wake si muziki wa hip hop tu. Mkali wa kupiga beatboxing kwa sana ni Michael Winslow kutoka katika filamu ya Police Academy.
Kwa vile imeibukia kutoka mjini South Bronx, utamaduni wa hip hop umeenea dunia nzima. Muziki wa hip hop
awali ulianzishwa na Ma-DJ waliokuwa wanatengeneza midundo kwa kutumia
mtindo wa kurudirudia na kusimama (hasa katika visehemu vidogo vya
muziki wa kusisitiza mwelekeo wa kigongoma) kwenye turntable mbili, hasa
hujulikana kama kusampo muziki.
Hii baadaye ikaja kusindikizwa na "rap", mtindo wa wizani unaotoa
maneno au mashairi yaliyo kwenye vipimo vya mstari ulalo wa nota 16
katika fremu ya muda, ikiwa sambamba na beatboxing, maujanja ya sauti
hutumika hasa katika kugezea mfumo wa midundo na elementi za muziki
mbalimbali na mautundu na vionjo kadhaa kutoka kwa Ma-DJ wa hip hop.
Muundo kamili wa kudansi na staili kadha wa kadha za mavazi zimezua
mashabiki miongoni mwao katika muziki mpya. Elementi hizi zimeonesha
mabadiliko ya na maendeleo kadha wa kadha katika historia ya utamaduni
huu. Baadhi ya miziki ya hip-Hop hutoa maelezo ya kisiasa.
Mahusiano baina ya graffiti na utamaduni wa hip hop unatokana
mionekano mipya tofauti iliyoongeza ufafanuzi wa kina na uenezi tofauti
wa kivitendo ambapo kwingine walichukulia elementi ya hip hop kama
sehemu ya sanaa, kukiwa na mpitilizo mkubwa baina ya hao wanaondika
graffiti na hao wanaotenda elementi zingine za hip hop kivyao. Leo hii,
graffiti imebakiwa kuwa sehemu ya hip hop, wakati kwa upande wa sanaa
imechukua eneo kubwa katika masuala ya picha na michoro katika maeneosho
mbalimbali duniani kote.
0 comments:
Post a Comment