background img

The New Stuff

KUTOKA KIJIWENI!!!__WATOTO WAZURI BONGO MOVIE NA HABARI ZA CHA-ARUSHA BUKU MBILI MOKO!!__BOFYA HAPA!! TULIBENEKE MTU WANGU_



 Lulu pichani
Moja ya vijiwe vya mitaani jengo bovu kwa dokta ama Pusha


 NA MWANA KIJIWE
Pita pita za kitaa zimenishusha pale karibu na Jengo bovu ama wenyewe wanapaita kwa Pusha ama Dokta nakuta wadau kadhaa wa kitaa cha juu nawapa hi!! nasikia mluzi kwa mbali kucheki ni mwana yuko juu ya Boxer siunajua si zile za ndani ni tukutuku ama waswahili wana mind niseme pikipiki haina noma basi poa ananiuliza vipi unaenda Ahhh!! niende wapi tena mwanaharakati wangu mi leo ni hapa hapa kijiweni tule nyuzii mbili tatu.
Linapita gari la kigogo mmoja serikalini mwana mmoja anaamua kudisi "Wale wale wezi wetu"
nashtuka kidogo nikaona sio kesi ngoja nijivute pande zake nimsikilize akashusha tuhuma kichizi juu ya mchakato wa kule dodoma kwa mjengo mtukufu wana wakmsapoti kwa neno moja tu Eeh!
mara akaja mwanaharakati mwingine na tukutuku spidi zakutosha na gazeti lake mkononi akaliweka kwenye moja ya matairi pale kjiweni.
kulitupia jicho kumbe ni moja ya magazeti yanayoongelea sana wale mastaa wetu mbele lina bonge ya picha ya mwanadada wa bongo movie yuko kama nusu utupu vile nikimfananisha na staa mmoja wa mamtoni kule.wakati naendelea licheki cheki lile gazeti mdau mmoja akaniambia braza apo utabaki kula kwa macho tuu nikashtuka kidogo Alaa!! kumbe kuna mdau ananichora kise***e apa.
jamaa akaendelea uku anatafuna tafuna vijiti vyake wenyewe wanasemaga anasaga ule mzigo haramu ama Gomba "awo nenda bongo pale ukiwa na mawe tu utawagonga adi utafurahi"
mwengine akadakia uko watoto kama Wolpa, Wema, Uwoya, Lulu, n.k ni wewe tu broo! nkaona sio kesi ngaja niwasikilize awa makamanda wangu leo
mara wadau wakatemana na ile stori ya mjengoni mada ikawa ndo hawa watoto wazuri kama Lulizo!
wa kule Brazili. Nikicheki saa kwenye kimeo changu ni saa 4 asubuhi wadau wako wakutosha apa kijiweni na siunajua tena suala la ajira ni sinema uku kwetu ikawa haina matatizo kabisa kwenye uchangiaji. Kila mtu alionesha umahiri wake daah!! kweli sisi wabongo tunapenda kungonoka.
basi pale tukawasifia hao watoto wee! adi mishale ya saa saba hivi dah!! ukubwani kukaanza kudai mazaga zaga nikacheki na wadau wakantonya kuwa mazaa karibu tutaenda muungisha nkaona ni mzuka.
Asa wakati tunajiandaa kwenda kufanya mchakato jamaa mmoja akaniambia nimtoe kitu kama buku mbili moko akafanye mchakato nikaona No sweti!! nikamtoa mwana uku bado namcheki nikamuona uyoo aazama jengo bovu mwana akanitonya anaenda kwa dokta uyoo hee kwa dokta..? ndiyo ama kwa pusha aaah! Ok nimekusoma baaria asa vpi kuhusu mlo uyu jamaa nikaambiwa tena apa baada ya stori uwa wadau wanaenda kuji busti kwanza ndo mishe nyingine zinaendelea.
sisi tukaenda kwa mazaa kumuungisha mihogo ilikua mitamu kinoma noma nikaona ngoja sasa nizame town nikafanye mitikasi mingine "Oyaa wana mida mida" ndo nikaagana na wana mmoja naye akawasha tukutuku yake ile boxer akanambia wapi man nikamjibu mi naenda town bila hiyana si unajua awa jamaa ni kambi kokote basi hawooo!! mpaka town nikampa mtonyo wake mimi nikaendelea na harakati zangu.

0 comments:

Popular Posts