NA MWANA KIJIWE
Katika tasnia inayoongoza kwa kukere walio na busara na maadili bongo basi huwenda ikawa ni hawa wachekeshaj wasio na uelewa mpana wa mambo duniani. Nasema hivyo nikiwa na akili timamu kabisa na kila mwenye akili timamu atanielewa ninacho maanisha hapa.
Tabia mbaya na kufuru kama sio dalili za usodoma Bongo ni ile ya wasanii hasa wamaigizo yakuchekesha Tanzania kujifanya kama wanawake kwa kuvaa nguo za kike tena hadi kupaka wanja na kufunga mawiji yani ukiwaona hutaona tofauti na wanawake eti kwa dai la kuchekesha au kufurahisha watazamaji wao mimi binafsi huwa nakereka sana na wala sipendelei kuangalia huo ujinga wenu.
Mnafikiri wadogo zenu wanaotaka kuja kuwa waigizaji wa komedi kama nyie wataanzia wapi kama sio kujivalisha hulka za kuwa kama wanawake mwishowe ni kuwa Mashoga kamili nasema hili kutokana na maudhi ninayoyaona kutoka kwenu wala msichukie mkiambiwa mnachochea ushoga nchini.
Tuchukue mfano mdogo wewe ni kaka au dada una mdogo wako wakiume anayependa kuwa mchekeshaji anayetoa ukweli kwa njia ya maigizo tena mahiri kama yule Joti wa makavu laivu. Akaamua kumfanya Joti kuwa ndio role model ama kioo kwake, siku moja ukamkuta amevalia kama mwanadada mbele ya kioo anajiongelesha kama huyo Joti. Vuta picha wewe kama mkubwa wake utamchukuliaje..?
Je, utamchukulia kama anayejifunza uchekeshaji au anaye jifunza tabia za kike 'ukike kike' ambao ni moja ya chimbuko la tabia ya ushoga kulingana na wanasaikolojia waliogawa ushoga katika makundi matatu makuu ambayo ni moja, Ushoga wakuzaliwa ambao unatokana na homoni Fulani Fulani mwilini, mbili ni ushoga unaotokana na kutaka kulipa visasi mfano mtu aliyetengwa na mzazi hususa ni wakiume (baba) na tatu ni ushoga tabia ambao huu utokana na mwanaume kuiga tabia za kike hii huweza kutokana na mwanaume kukaa sana na dada, mama au rafiki wa kike sana hapa itambulike sio mpenzi wa kike.
Basi kutokana na maelezo na chambuzi za wanasakolojia hao tatizo hili la wachekeshaji wetu kufanya au kuupigia debe vitendo vya ushoga labda wakijua au kwa kutokujua. Wako wengi hususa ni hawa wa vikundi vifuatavyo moja ni hawa walioko kwenye Ze comedy Orignal na pili na wale wa Ze comedy. Nimeamua kuwataja wazibila kuficha kwani kwa kweli mmekuwa mkikera sana
Embu make na kujiuliza nini huwa kinawafanya mpaka mjifanye kuwa kama wanawake..? ni pesa au ni ulimbukeni Fulani umewavamia...? je hizi picha zenu zikichukuliwa na kuwekwa kwenye mitandao ya mashoga duniani mtajitetea kwa lipi mbele ya jamii..? kwani hakuna wachekeshaji wa kike nchini wakaigiza izo sehemu...? embu amkeni achene ulimbukeni
hivyo neno langu au ushauri wangu kwa hawa wachekeshaji nchini ni kuacha mara moja tabia hiyo mbaya na kutafuta wachekeshaji wanawake mfano mzuri ni Mizengwe ya ITV hawa mimi naweza waita moja ya waigizaji makini na wenye kujua nini adhari ya uchekeshaji na muonekano wao mbele ya jamii
AMKA MTANZANIA!!
0 comments:
Post a Comment