background img

The New Stuff

LEO KUNANI!!__HEPII BETHI DEI MISTA PREZIDENTI ZAWADI YANGU KWAKO NI KIDOGO NILICHONACHO KWENYE HII HEKAYA!!?__ BOFYA HAPA KUISOMA


NA MWANA HEKAYA
Leo ni tarehe 7 ya mwezi wa kumi kwenye mapito yangu niliyowahi kuyapiti pitia nilipata ksikia eti! namba 7 ni namba kamilifu Zaidi hadi kwenye vitabu vya dini. Hapo sina uhakika sana ila ni ninasikia sikia tu waungwana.

Leo ni moja ya siku nilizopata kuzisikia na pia kuzisoma kuwa mweshimiwa mkuu wa nchi yetu ndio kazaliwa je wewe unaliua hili? Napata mashaka na uzalendo wako kama unashindwa kuijua tarehe aliyozaliwa mkuu wako wa nchi ila zile za watu kama Baroteli na Lil wayne zipo kichwani tena hadi histora zao zilizofichwa fichwa.

Ila dhumun langu halikuwa kuongela hayo bali hapo nilikuwa nakukumbusha tu na wewe ujipime namna gani hufuatilii mambo muhimu hapa bongo kwani ni uwongo?. Nisipende kukuchosha na kukuudhi buree maana sisi wabongo huwa ukweli kwetu sumu hadi tukaweka kamsemo huku tukiwasingizia wahenga eti "UKWELI UNAUMA!'' umeona sasa sisi tulivyo watu wa ajabu

Basi Mista prezidenti hili ndilo tatizo letu kubwa wananchi wako kupotosha potosha mambo hasa mazuri na kuyageuza yawe mabaya kwa sababu zetu binafsi mwisho wa siku yanatuumbua sisi sisi. Nakumbuka kipindi nasoma shule ya msingi kama sikosei ilikuwa na darasa la pili hivi nikasomaga kitabu cha taasisi vile vya rangi ya machungwa na kweli vilikuwa ni machungwa sababu tulivipenda sana basi kule ndani kuna hadithi Fulani nakumbuka tu kakipande kadogo kalichonifanya nikajifunza mambo mengi hadi leo

Kile kipande kinasema hivi " Samaki wangu jikoni nikatoka nje bwana kumuuliza paka wangu akajibu nyau! nyau!!" hichi kipande na uhakika ukimuuliza hata mheshimiwa Ridhiwani atakuwa anakikumbuka vyema kama alikisoma hichi kitabu. Hichi nikipande kidogo sana ila kina maana kubwa kwa mustakabali wetu kama taifa hivi leo

Bunge maalumu la katiba limeisha salama hilo hata mimi linaniurahisha japo kuna mambo mengi yametokea hapo katikati lakini bado nafarijika kuona kuwa siyo mambo ya ajabu sana kwani yalikuwa yatokee tu hapo tena nawakumbuka wahenga na kauli zao eti "HATA VIKOMBE VINAGONGANA KABATINI" ila wasi wasi wangu ni juu ya kuendelea kugongana hadi nje ya kabati.

Ngoja nitafute msemo wa wahenga niweze kujifariji kidogo Mista prezidenti...(kimya kidogo huku natafakari) Nimekosa mheshimiwa ila natumaini wewe siyo kama yule mfalme LA! LA! LAH! nimemkumbuka ghafla yule mfalme wa kwenye kile kitabu cha darasa la tatu kama sikosei ina hakika kama mpaka leo kinatumika kile kile.

Mista presidenti hebu ngoja nikupe simulizi kidogo ya kile kitabu "Kulikuwa na mfalme mmoja bas alikuwa anapenda sana vitendawili siku moja aliandaa ni shindano kama sijakosea na atakaye shinda angemuoa binti yake, Basi vijana walienda kwenye shindano wengi sana ila wengi walishindwa na kama sijakosea walikuwa wauliwe. Ila kuna kijana mmoja yeye alivyoenda kwenye shindano alienda na chupa yenye nge' aliwato kwenye miembe wale!.... Basi mfalme aliamiwa aingize mkono kwenye ile chupa weee!!! yani alibaki kusema tu La! la! lah! basi wengi shuleni tukakariri mfalme la! la! lah! badala ya Malme anayependa vitendawili.

Nikiwa sekondari Mista prezidenti niliambiwa kuwa fasihi huishi hata miaka elfu moja! nilishangaa sana kivipi ili hali siyo kiumbe basi kama ni kiumbe kitakua cha ajabu sana, na kweli bhana hii simulizi ya mfalme La!la! lah! naiona leo kule Dodoma ila sina wasiwasi tena kwani shindano limeisha.

Mista prezidenti tumeongea mambo mengi sana mimi na wewe na naamini umenisikiliza vyema ila mimi nina ombi moja tu kwako kwani najua wewe ni mdau mkubwa wa vijana ila huku kwetu hali siyo nzuri kabisa si unaukumbuka ule usemi wa hawa wahenga eti "MKONO MTUPU HAULAMBWI" basi unaumaliza sana vijana kwenye suala la ajira nakumbuka na wewe ni mkerwa wa rushwa na wazi wazi ulitukumbusha kuwa rushwa ni adui wa haki na tumemuongeza kama adui wa taifa pia hapo hongereni sana wakubwa.

Mimi nimalizie kwa kuzidi kukutakia maisha marefu yenye furaha hapa duniani ngoja nikaendelee na shuhuli za kujenga uchumi wetu, tena nimekumbuka kitu mista prezidenti mimi nadhani sasa tubadili hii kauli isiwe kujenga nchi tena bali iwe kujenga uchumi wetu maana vijana wengi wanashangaa mbona hii nchi imesha umbwa na Mungu sasa tujenge nini tena?

Kazi njema Mista prezidenti na Asante kwa kunisikiliza!

0 comments:

Popular Posts