background img

The New Stuff

OLD SKULI YA DJ BONNY LUV NA DJS WA ENZI HIZO!!

Linapokuja suala la oldies. Nakukumbuka sana wakati baadhi ya Djs walipofanya vitu vyao kwenye club mbalimbali hapa nchini.
Pamoja na muziki huu nyakati Fulani kuanza kupoteza ladha kutokana na kusahaulika lakini namshukuru mkongwe Bonny Luv, ni miongoni mwa Djs walioendeleza oldies nakumbuka pale Latervena.
Basi mbali ya Dj Bonny Luv ambaye bado ameweza kuhudumu katika fani ya muziki mpaka sasa wapo wengine kama Young Millionaire, Richie Dillon, Jerry Kotto, Bush Doctor, Eddie Grand,
Sure Boy, Choggy Sly, Kalikali, Mr. A wa pale Continental Club Mix, Chris Phabby The Lover.

Pia nakumbuka sana huwezi kutaja historia ya disco Tanzania bila kutaja kumbi kama Mbowe Club sasa hivi Club Billicanas, Maggot Ushirika, Rungwe Oceanic, Kilimanjaro Pool Side, Msasani Beach Club, Lan’gata, Mwanza tulikua na Kabibi, Savanna, Alshers, Natta Hotel, Pamba Roof, Rendevous Makutano Mwanza Hotel, Uptown Disco, Cave Disco Arusha, Kilimanjaro Disco pale Moshi, NK Disco Dodoma. Kulikua na makundi ya vijana wa Disco kama ILALA FOURWAYS BROTHERS, SWEET CORNER hilo ndilo kundi alilokuwa anachezea disco huyu jamaa anayemiliki sasa hivi studio ya BAUCHA RECORDS, Ally Baucha. Mussa Simba aka Black Moses, Athuman Digadiga, Ommy Sidney walikuwa wakichuana vikali pale Lan’gata Social Hall Kinondoni enzi hizo!

nyimbo za oldieS:
1.HEART & SOUL wa PROJECTION.
2.SKIPS A BEAT wa WARP NINE.
3.LOST YOUR NUMBER wa NUSHUUZ
4.WARM LOVE wa BEATMASTERS.
5.TREAT HER LIKE A LADY wa TEMPTATION.
Jamani the list is endless hizo ni baadhi tu ya kali za enzi hizo. OLD SKOOL WILL ALWAYS REMAIN THE BEST SKOOL!
……………………………..
Enzi hizo ukienda Rungwe Oceanic Beach Resort ya Mzee Mwakitwange ulikuwa unakuitana na majina kama vile DJ Ngomely, DJ Pop Juice na wengine. Ukisogea jirani na hapo Rungwe, yaani Silver Sands, unakutana na kina John Peter Pantalakis, Choggy Sly na Kalikali ambaye baadaye alihamia YMCA.
Ukienda Africana ulikuwa huangalii simba aliyekuwa anafugwa hapo, bali pia DJ Mehboob, wakati ukishuka mjini hususan Motel Agip na baadaye New Africa hotel ghorofa ya saba kulikuwa na DJ Emperor (huyu Joseph Kusaga bosi wa Clouds 88.4 fmunaemjuea), Boniface kilosa a.k.a Bonny Love na DJ Jesse Malongo (wa Club Afrique, London).

Baadaye kidogo ikaja Space 1900 iliyoanzia hoteli ya Mbowe na kuhamia YMCA, na kuleta ushindani mkubwa kwenye fani ya muziki ambapo disko lilifunika kabisa muziki wa dansi. Vile vile ikazuka New Vision ambako DJ Super Deo, DJ Paul MacGhee na Joe Johnson Holela walitengeneza majina sio kawaida, huku wakimpa darasa DJ Young Millionaire ambaye wakati Fulani tulikua naye katika studio za Radio Free Africa na Star TV.
Baada ya Space 1900 discotheque kuhamia YMCA, disko la RSVP Discotheque likazaliwa Mbowe na Ma DJ wake walikuwa mkongwe Saidi Mknadara a.k.a DJ Seydou, akisaidiana na DJ Yaphet Kotto.

Kwa ufupi, pamoja na kwamba DJ Eddy Sally na DJ Sweet Francis wa hoteli ya Keys mtaa wa Uhuru walikuwa juu kwa vyombo vya kwanza vya kisasa vya disko, lakini ni DJ Seydou na DJ Yaphet Kotto ambao ndio walikuwa vinara pale RSVP Mbowe. Yaani baada ya kuruka majoka kila sehemu uijuayo, lakini vijana wote wa Dar walikuwa wanakwenda Mbowe kumalizia usiku kwa DJ Seydou na DJ Kotto.
Kwa ufupi huyu ndiye aliyekuwa baba wa disko Dar, sio pekee kwa uwezo usio wa kawaida wa kupanga muziki tu bali pia ngekewa ya kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote nchini.
……………………………….

kilikuwa kipindi cha disco haswa kuanzia New York (Saturday Night Fever). Kati ya mwaka 1978 na 1985 baada ya hapo Break Dance.
Na Ikumbukwe Kotto na Seydou. Madj hawa wawili walikuja na staili mpya kabisa ya kupiga chapati (santuri) na dawa za mbu (kanda) huku wakidansi behind the Dj desk. Kwa mtakao kuwa mnakumbuka mtakumbuka ndiyo waliokuwa madj waliokuwa wanachoreography dansi zao na wanaovaa sare ya kazi maovaroli. Jamaa walikuwa watamu sana.
Kama sijakosea mwaka 1982 au 83 likavuma JeSet Disco na Dj Rusual na Baadaye Young Omar, Msasani Beach Club. Ninaweza kusema mpaka sasa hivi katika historia ya burudani ya muziki hakuna disko wala bendi lililowahi kutengeneza matangazo makali kama JetSet Disco.
…………………………………………

THIS REAL REMINDS ME ON OUR GOOD OLD DAYS!!! HAKIKA MCHANGO WA DJ SEYDOU KTK FANI YA DISCO HAPA NCHINI NA EAST AFRICA KWA UJUMLA NI WA KUKUMBUKWA DAIMA..MENGI YAMEZUNGUMZWA NA WALIONITANGULIA LAKINI NAPENDA KUELEZA PASIPO KUUMA MANENO KUWA DJ SEYDOU NA WENZAKE WA ZAMA HIZO WALIKUWA NI WATU BRIGHT KWELIKWELI..:
1. WALITAMBUA KWAMBA DHAMANA YA STAREHE YETU VIJANA NA WAZEE WAPENDAO DISCO ENZI HIZO ILIKUWA MIKONONI MWAO.
2. WALIUKUBALI NA KUUHESHIMU WAJIBU HUO.
3. MARA ZOTE WAO (DJs) WALIKUWA WAKISHINDANA KURIDHISHA WAPENZI/MASHABIKI WA DISCO.
4. SIKUWAHI KUSIKIA BIFU ZA KIPUUZI BAINA YAO KAMA ILIVYO KWA WADOGO ZETU SASA HIVI. BIFU YAO KUBWA ILIKUWA NI KUWAHI KUPATA VIGONGO VIPYA ILI KUKONGA NYOYO ZETU. NA KWA HILI WALIFANIKIWA SANA TENA SANA.
5. KWA KUFIKIRIA HALI NGUMU YA MAWASILIANO BAINA YA TANZANIA NA NCHI NYINGINE DUNIANI KULINGANISHA NA SASA HIVI, NAAMINI UTAKUBALIANA NAMI KUWA WATU HAWA (DJs) WALIFANYA KAZI KWELIKWELI HIVYO KUTHIBITISHA PASIPO SHAKA BRIGHTNESS YAO.
6. WALIIPENDA, WALIIMUDU NA WALIIHESHIMU SANA FANI YA DISCO. MARA ZOTE WALIAMINI KUWA KUTUTUMIKIA SISI WAPENZI WA DISCO ILIKUWA NI WAJIBU WAO. NA KTK KUTEKELEZA WAJIBU WAO HUO KWA HAKIKA ILIWAJENGEA HESHIMA KUBWA, NA HATA LEO TUNAWAHESHIMU NA TUNAWAPENDA SANA.
7. KAZI ZAO ZILITUUNGANISHA VIJANA NCHI NZIMA. TUKAJUANA, TUKAPENDANA NA HATA WENGINE TUKAWA KTK UCHUMBA NA HATA LEO NI WANANDOA HALALI NA FAMILIA ZENYE KUHESHIMIANA NA KUHESHIMIKA. HAYA NI YA KWELI;
WADOGO ZANGU (DJs WA SASA) JIFUNZENI KWA KAKA ZENU HAWA ILI MREJESHE HADHI YA DISCO NCHINI. NI HAZINA KUU KTK MEDANI.

0 comments:

Post a Comment