background img

The New Stuff

‘Ben Pol’ aliachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Jikubali’, Juni mosi.

MSANII wa muziki wa miondoko ya R'n'B, nchini, Bernard Paul ‘Ben Pol’ aliachia video ya wimbo wake mpya wa ‘Jikubali’, Juni mosi.
Akinukuliwa na moja ya kituo cha redio nchini mwishoni mwa wiki, Ben Pol alisema ujio wa video hiyo ilikuwa faraja kwa wadau wa muziki wake hapa nchini na nje ya nchi.

“Singo ya ‘Jikubali’ imepokewa kwa mikono miwili, hivyo nina imani na hata video hii itapokewa hivyo hivyo, zaidi naomba sapoti ya mashabiki,” alisema Ben Pol.
Aliongeza kuwa video hiyo aliyoitengenezea jijini Arusha chini ya muongozaji wake Nisher, itakuwa moto mkali katika vituo vingi vya televisheni kutokana na ubora wa hali ya juu.

Wakati huo huo, Ben Pol amewaomba mashabiki wake kutumia wiki hii ya mwisho ya upigaji kura katika tuzo za Kilimanjaro kwa kuhakikisha wanampigia ili aweze kunyakuwa tuzo hizo na hatimaye aweke historia ya kuwa msanii wa kwanza wa RnB kunyakua tuzo nyingi.

0 comments:

Popular Posts