Diamond Platnums akiwa ni miongoni wa abiria waliokwama kutokana na
uwanja wa ndege wa Jomo Kenyata kulipuliwa leo alfajiri, ameiambia
millardayo.com kwamba imebidi abiria wapelekwe hotelini na kuambiwa
inawezekana ndege zikaanza kuruka saa moja au saa mbili usiku leo ambapo
taarifa walizozisikia ni kwamba ni shambulio la bomu. Kwa sasa imetangazwa abiria wako salama ambapo ndege zote zilizokua zinatua Nairobi zimeelekezwa kutua Mombasa.
KWA
TAARIFA YAKO: Tarehe kama ya leo 07/08 mwaka 1998, Balozi za Marekani
nchini Kenya na Tanzania zililipuliwa kwa milipuko ya mabomu. Ni miaka
15 imepita sasa.
Leo, tarehe 07/08/2013, Uwanja wa ndege wa
Kimataifa wa Jomo Kenyatta umekumbwa na janga kubwa la moto. Hizi ni
tarehe mbili kubwa zenye historia kwa nchi ya Kenya.
Tunaungana na Wakenya kutoa pole kwa janga hili lililowakuta. Ungana nasi kutoa pole.
0 comments:
Post a Comment