background img

The New Stuff

Staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mwanaye Paula Paul

Staa wa filamu za Kibongo, Kajala Masanja na mwanaye Paula Paul wamekuwa kama mtu na mdogo wake kutokana na kulingana vimo na kufuatana kila kona kiasi cha kuzua maswali kwa watu. Hivi karibuni wawili hao waliambatana kwenye mwaliko wa futari iliyoandaliwa na msanii wa filamu, Aunt Ezekiel na kuwafanya mastaa wengine kudhani ni mtu na mdogo wake. “Ni vigumu kuamini kama huyu ni mwanao, miye nilipomuana nilidhani umekuja na mdogo wako, kweli kuzaa mapema ni mali,” alisema msanii Devota Mbaga kwa niaba ya wengine waliokuwa wakishangaa.

0 comments:

Popular Posts