KUTOKA KIJIWENI!!!__STAA BONGO? PESA, NYUMBA NA GARI VYOTE VYA SHUGA MAMII TOWN__BOFYA HAPA KUJUA NANI KASEMA!!?
NA MWANA KIJIWE
Nikiwa katika misele yangu leo town si unajua mwenenu leo niko off sina dili na wakubwa wa kaya nikaona sio kesi kubwa kama nitapozi town kwa masela zangu tuliokuwa nao skuli Enzi zile za "jua lilee literemke mama!! aiyaaa!! iyaa!! iyaa! mamaaa!!!" wewe uliziimba hizinyimbo kweli..? asa ndo ujue nikikwambia Zee ujue si lakitoto.
Nakumbka Enzi zile mwenetu mmoja alikuwa akilipiga lile ngoma kubwa apo sisi niku troti kama jeshi Fulani hivi kumkabili yule nduli ujinga!! apo Zee nimeua au sio..? yah!! mwanangumwenyewe si unakumbuka faza wa nesheni alishasemaga ujinga ni adui asa sisi asubuhi asubuhi tukawa tuna pasha kumkabili kikomando ilikuwa ni ishu sana kipindi ile tunazama class wenyewe tulikuwa tunakuita clangaa.
Iyo ilikuwa ni shoti introdakisheni toka kwa Zee, basi nikapiga pasi ndefu apo rodi niko napiga bonge ya maatua kama nawai dili kubwa town maana hukawii kuitwa mzururaji huku town afu Zee simaindi hizo wala nini. Dakika kama ishirini hivi nikawa nimeshaibuka pande za wanangu ujue hawa wana tulipotezana kipindi kirefu kinoma yani sasa tumekuwa madingi kabisa.
Salamu mbili tatu Zee nikaona dizaini wana siku hizi wako bize sana namichakato ya maisha hadi wamenipita Zee lao kipindi kile basi ndio nilikuwa mjanja wao siunajua zile zakiskuli watoto wazuri unaambiwa Zee ndio nilikuwa nawatongozea masala pale clangaa!. Ujanja wote wa laifu ulikuwa umepiga kambi kwangu yani ndio jina la ticha likawa langu.
Stori mbili tatu za maisha sio utani wana ni gudi laifu kinoma si ndiyo Zee nikataka kujua haukamzi wana wametusua kifasta fasta hivyo hapa town..ndio wanawakanitonya Zee mjini mipango tu kila kitu ni posibo. Nikaona isiwe shobo sana nikawateli wanipe ramani mbili tatu chapu ujue Zee ninausongo na pesa!!?
Mwana hakuwa na zile za kiboya akanipa mchongo kama hivi yani "Ujue Zee pale kitaa chenu kuna mitaji kama mitatu hivi" Zee nikatega sikio ki kubwa sasa ili mwana afunguke frii..."kuna ule wenye noah nyeusi mnene mnene mwingine ni yule wa Benki sista sista flani ana Karna ya bluu na kuna yule mwenye ile supa market.." Kwanza Zee nikashituka kidogo haukamzi huyu mwana ana koneksheni na watu wakubwa kama hawa..? ujuewote aliowataja ni vigogo wa mtaa wetu pale ila Zee nikaona ngoja niwe mpole kwanza si unajua ukitaka kujua kuwa mpole ata kwa wichi dokta kwenyewe wana wanaambiwaga wawe wapole.
Mwana akanitonya Zee mi bado damu nyepesi nikapige mzigo pale ila kivipi akati Zee digrii yangu ni yakuongea tu madude yateme yenyewe, mwana akanona naleta zile za kitoto akafunguka laivu unaambiwa eti wale ni mashuga mama hapa town. kitu kama fayaaa vile kikapasi top mpaka dauni nikakauka kwanza fasta fasta nikajiuliza kumbe hivi ndo dili za wana siku hizi ..?
msela akafunguka Zaidi yani unaambiwa awa wadogo zetu wanao hit uko kwenye redio mara kesho kesho kutwa ana ndika rodi wanazitolea huko yani kwa mashuga mamii town. uajua dizaini Zee nikaona wana wamebugi ishu Fulani za ki'laifu
nikawacheki wana pale dah!! kumbe nao ni wake za watu..? kwani mtu aliyeolewa si ndiyo mke mwenetu..? asa Zee siwezi kaa na wake za watu nisije pewa kesi ya kuchepuka buree
nkatembeza gwarakwa wanangu ile kuwachomoka kiteknologia nikawapa mchongo nilikuwa napita tuu kuna ishu nafukuzia apo kati dizaini mwana kanitumia meseji ngoja nimuwahi iyo ishu tutakuja ibonga wani dei...
Zee huyooo! nikaacha manyoya tu!! badae mwenetu.
0 comments:
Post a Comment