background img

The New Stuff

SAKATA KATIBA MPYA___MHESHIMIWA MCHUNGAJI PETER MSIGWA AMVAA PROFESA ISSA SHIVJI JUU YA UZALENDO WAKE!?__BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI


DURU ZA KISIASA
Akihojiwa kupitia kituo cha televisheni ITVProf. Shivji alielezea mantiki yake katka nini hasa maana ya neon Uzalendo kwake, ambapo alieleza kuwa uzalendo ni kuitii serekali iliyopo madarakani na utaifa ni ukereketwa kwa nchi yakohata kama huipendi serikali iliyopo madarakani..

Akimkosoa mwana taaluma huyo mheshimiwa mchungaji Peter Msigwa mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chadema ame posti haya katika ukurasa wake wa Facebook, nanukuu

"Kwa HESHIMA zote , napinga mtazamo wa prof. Issa Shivji , kuwa eti, uzalendo ni kuitii serikali iliyokomadarani. Na utaifa eti ni ukereketwa wa nchi yako hata Kama huipendi serikali.
Kwa mtazamo huu , Nyerere hakuwa mzalendo kwa kuwa aliipinga serikali ya mkoloni ?.
Vipi Mandela aliyepinga serikali ya kibaguzi kule bondeni naye hakuwa mzalendo?
Vipi waganda walioipinga serikali ya Idd Amini?
Vipi serikali Kama ya Mabutu wa DRC?...
Kuna wakati kuichukia serikali serikali iliyopo madarakani ni uzalendo ,serikali huja na kuondoka, ila taifa hubaki, serikali yoyote ambayo ,inatumia vibaya raslimali za nchi yake,ikichukiwa ni uzalendo.
Serikali ya kifisadi, inayoendekeza ujangili, wizi na uporaji wa Mali za umaa inafaa kuchukiwa kwa nguvu zote na huo ndio uzalendo.
Serikali inayokiuka haki za binadamu , inayokandamiza demokrasia ,kuitii serikali Kama hiyo sio uzalendo.
Ndugu Issa Shivji... Sijakuelewa hasa msomi Kama wewe. ..how would you say that ?saw you on news yesterday (ITV)."


Mwisho wa kunukuu. katika ost hiyo ya mheshimiwa mchungaji Peter Msigwa kumekuwa na comments zenye mitazamo mbali mbali huku mingine ikiwa yakuunga mkono wazo la Prof. Shivji na hata Mchungaji Msigwa. Yapi maoni yako? Bofya hapa! ku comment

0 comments:

Popular Posts