background img

The New Stuff

Ah! NIONGEZEE (1)


‘Salio lako jipya ni Tsh. 200,050. Umepokea Tsh. 200,000 kutoka kwa 255652XXXXXXX-Ashura, kumbukumbu no. PP172XXXXXXXX.F5463XXXXX 30/01/2017’ Ni ujumbe ulioingia kwenye simu ya Abuye huku akiilaani sauti ya sms iliyoingia alizidi kuuvuta usingzi uliokuwa umemuelemea baada ya uchovu wa pilika pilika za siku nzima. Dakika si nyingi si unaujua wasi wasi wa mtu aliyetuma pesa mahali alafu asipate jibu la kupkelewa au la! Basi ndio wasi wasi uliompata Ashura ambaye wakati huo alikuwa amejilaza kitandani kwake huku kanga moja ikiusitiri mwili wake uliopendezeshwa na rangi nyeupe, mtoto wa kisambaa aliyekulia Tanga mjini akaanzisha maisha yake jijini Dar es Salaam baada ya kupata kazi shirika moja la kimataifa. Ki ukweli Ashura alijaaliwa maisha mazuri tangu utoto wake hakuijua shida, hakuwai kuomba kitu akakikosa kwa wazazi wake ila dunia haina mwenyewe Ashura alikuwa na njaaa moja tu! Njaa ya mapenzi. Haikuwa rahisi kuamini kama binti mrembo kama Ashura angeweza kuwa na njaa ya mapenzi, vile alivyokuwa mrembo kila mwanaume alimtamani na kuishia hapo hapo kumtamani kwani waliamini lazima angekuwa mke wa kigogo Fulani na kumtongoza ni kujitafutia kifo mwenyewe.

Msitu haukosi wanyama wakorofi, Abuye kijana wa Sinza wenyewe wanapaita Sinza kwa wajanja Alisha ugusa moyo wa Ashura mchana wa siku hiyo. Ashura akiwa amejilaza  kitandani aliukumbuka mchana wake namna ulivyokumbwa na mshituko wa furaha, ni akiwa ametokea Bank alipokuwa ameenda kuonana na meneja wa bank ndipo alikutana na hali aliyombadilishia siku yake. Akiwa anaelekea kwenye gari lake aina ya IST ghafla alitokea kijana ambaye hata yeye hakujua alipotokea na kumwambia ‘dada umependeza’ ni maneno hayo mawili tu yalitosha kumsisimua hadi kope za macho yake kwa mshangao uliochanganyika na woga. Akionekana kama asiyejali yatokanayo na kauli yake Yule kijana alimuangalia Ashura na kasha kutabasamu huku akielekea ndani ya bank.
Ashura hakuacha kumtazama yule kijana huku akitingisha kichwa na kutabasamu alifungua mlango wa gari na kuvuta pumzi ndefu huku ameshikilia usukani kwa mikono miwili kama mtu aliyekuwa akijinyoosha viungo vya mwili. Hakuweza kuwasha gari muda ule, alimtafakari Yule kijana kwa namna alivyokuwa na ujasiri uliojaa masihara kasha akaitafakari kauli yake, dada umependeza, akatafakari ni lini mara ya mwisho kuabiwa kauli kama hiyo hakika hakuikumbuka siku ya mwisho kuambiwa kauli ile, akatabasamu ena huku akijichekesha mwenyewe na kujiandaa kuianza safari yake. Zilikuwa zimeshapita karibu dakika 6 dakika zilizotosha kumfanya Yule kijana awe tayari ametoka ndani ya ile bank, Ashura akiwa bize kutoa gari kwenye parking alishaanza kumsahau Yule kijana hadi alipofika kwenye geti wakati akikabidhi kikadi alichopewa na mlinzi getini ndipo akamuona Yule kijana akiwa amesimama anaongea na boda boda.

‘Kaka twende!’ ni sauti nyembamba nzuri ya mrembo ikitokea kwenye gari ilimuongelesha Yule kijana aliyeonekana kama kuto kuijali sana huku akizidi kuongea na boda boda.
‘Bro sista ako anakuita kule’ alisema Yule boda boda kumwambia Yule kijana
‘Mpotezee bhana mimi simjui ata’ alisema Yule kijana huku akiwa anachezea chezea ndevu za kidevu chake. Baada ya kuisikia honi kutoka kwenye gari la Ashura Yule kijana hakuwa na ujanja mwingine zaidi ya kumsogelea Ashura kwenye gari.
‘Kaka mambo?, pakia kwenye gari mwaya’ alisema Ashura huku akitabasamu,
‘Asante sista ila nipo na Yule boda boda’ alijitetea yule kijana,
‘Haya sawa asante kwa kukataa lift yangu’ alisema Ashura kwa unyonge huku akimuangalia Yule kijana, ‘Ah! Sista, usiwe mnyonge hivyo bhana unaupoteza uzuri wako’ huku akiwa na tabasamu alimwambia Ashura huku akimdadisi zaidi. Akihisi kama mapigo ya moyo yamebadilika Ashura alichukua pochi yake na kutoa kadi yenye mawasiliano yake na kumpatia Yule kijana,
‘Mimi naitwa Ashura, nipo pale UN, karibu siku moja kunitembelea’ alisema Ashura huku akimkabidhi ile kadi.
‘Poa sista mimi naitwa Abuye, baadae nitaku text upate namba zangu zinaishiwa na 52’ alisema Abuye akitabasamu.


Njiani Ashura alizidi kumtafakari Abuye huku akijisemea mwenyewe Abuye uwahi kunitext jamani’. Baada ya kufika ofisini Ashura alizidi kuisubiri sms ya Abuye kwa hamu, kila ilipoingia sms aliiangalia kwa haraka hadi ilipofika mida ya saa saba ilipoingia sms, ‘mamb vp sista, hii ndio namba yangu Abuye’. Huku akitabasamu Ashura aliisave ile namba na kuijibu ile sms.

Inaendele...

0 comments:

Popular Posts