background img

The New Stuff

PICHA ZA GIGY MONEY ZA TESA TENA MITANDAO NI ZILE ZA SUPU NA MATONYA!!



Na Trojan Maujanja.

Adje mwanangu mwenyewe?, hivi umeshadaka mchongo wa Gigy Pesa au mwenyewe anajiita Gigy Money, usiule upi ena bhana mbona unanikausha mwanao ki ivyoo? si ule wa Supu au? Ee!! huo huo mwenetu sasa kama unataka mwanao niuweke hapa wewe nitulizie kidogo tu mwanao nitakuletea huo mzigo ful full wala usiwaze mwenetu.

ila leo nataka nikupe ka stori kalichomtokea mwanangu mmoja si unajua tena wale wakitaa wanavyozinguaa ila ujue mwenetu kuna maraia weneyewe wanajiitaga raia weneye hasira kali daa!! usiombe siku waziamshie kwako we mwenyewe mbona utalowa tu mwenetu au uongo kwani? umeona ee unaambiwa mwana kachomoka mtaa wa kwanza wapili wa tatu tu kakutana na bonge la toto wenyewe wanawaita supu siku hizi, hahah!! raia bhana eti supu! ila ene wei ngoja na sisi tulichukue ilo supu.

basi mwana yeye kama wadau wengine si unajua supu dawa yake ni kulinywa tu! sasa mwana akajitia yeey ndio mwenye njaa sana na izo supu, akaleta ubia pale blaa blaa nyingi fulu kukenua meno motto kakauka tu!! ujue mwanao nakupaga michongo kibao ila ni dizaini ile ya Donti trai ati homu!! ki mieleka mieleka umenisoma ee? hapo barida mwenetu.

basi mchizi akaaanza kukumbuka michongo ya Trojan hapa kitaa media, si unajua tena basi mwana akaanza aplai mbinu pale motto wapii kala buyu tu, mwana akaona sasa hii miyeyusho akaamua mshika motto mkono ujue kuna wana watelebani kinoma mwenetu, motto akaona sasa huyu mchizi dizaini kazidi uboya si akaamua kuwaka na yeye acha amuunguze mwana, kweli hawa supu dizaini ilikuwa yamoto.

kujiongeza ujue ndio kanuni yetu mwenetu wewe ukiamua kuwa kama mwanao Trojan wewe uwe unajiongeza tu mbon mambo yote yatakuwa upepo tu mwenetu, sasa huyu mwana dizaini hii kanuni aliitia kapuni sasa sikilizia kilichompata. ile motto kumuunguza tu ujue mtu mzima lazima u thinki ki Ben Kason sasa mwana dizaini ali dilei acha wakora wamwamkie mwenetu, unaambiwa usichezee mashine gan ni faya tu!!.

mara Ohho! mbakaji, mara Oh! nyie ndio mnatuharibia watoto, Oh! mbakaji wa gesti, duh! maneno kibao yani mwana kabebeshwa ujue bora wangekuwa wanaongea tu asa wataongeaje kimya kimya bila kichapo kwa mfano? wewe uncheza na raia wenye ma Angri yao mwenetu? acha utani wewe mwana alichezea vya ushogo kwanza kama sitini hivi achilia mbali za maeneo mengineo yanayouma.

mwana kujitetea tetea pale raia wenye hasira zao wakaona sasa waende mapumziko kwanza mwana nae apate upenyo wakuingiza uwanjani sehemu za mwili zilizokuwa sabu, basi mwana akaji expleini pale raia wakaona ene wei kajiexplein alafu samutimu siyo ishu sana kuwazuia vijana wakaona wamwache atembee zake. Mwana kupiga jicho huku na kule kamwona motto amekaa pale pale raia wenye hasira zao walikuwa wamekaa wana piga maji.

Mwana ndio kusanuka kumbe hii supu ilikuwa ishaagizwa kitambo alafu yeye akaleta shobo, ujue mwanetu samutimu ukiona toto kala gunzi wewe tafuta utaratibu tu ujikatae mapema usije kuwekwa uwanjani kama mwenetu huyu kisa shobo zako tu!. ila kwa nini kwa mfano ujikatae wakati wewe ni legendi kitaa chenu pale, kwani wewe huonagi majogoo hata iwe vipi litakimbiza tu hahah!! ila ndio hivyo samutime uwe makini kimtindo mwenetu supu tamu ila nyingine za kitimoto afu wewe motto wa shekh unaanzaje kuzinywa kwa mfano?. umeon ee!! basi kama vipi badae mwenetu mimi nilikuwa napita tu kuacha hili tori manzee!!.



0 comments:

Popular Posts