background img

The New Stuff

Ifahamu Rau na Mo town kwa kifupi

Rau ni jina la kata ya Wilaya ya Moshi Mijini katika Mkoa wa Kilimanjaro, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 11,529 waishio humo.
Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002, mji wa Moshi una wakazi wapatao 144,739 .


 Kabila linaloongoza kwa idadi ya wakazi wa mji wa Moshi ni Wachagga wakifuatiwa na wapare na makabila mengine yaliyohamia kutoka sehemu mbalimbali za tanzania kama wasambaa,warangi n.k. Wachagga wanapenda vyakula vinavyopikwa kwa kutumia ndizi kama vile mtori, kitawa, na machalari.

Wakazi wengi wa Moshi ni wakulima, wafugaji na wafanyabiashara. Watu wengi wanaenda Moshi kufanya kazi na kurudi nyumbani jioni.Ukuaji wa mji wa Moshi hauendani na mipango halisi ya 'Mipango Miji'. Hii inatokana na kutokufuatiliwa kwa sheria mbalimbali zinazohusu uendelezaji wa miji.Moshi ni mji wenye baridi katika miezi ya Juni mpaka Agosti na kipindi cha joto katika miezi ya Oktoba hadi katikati ya Januari.

 Mji wa Moshi una mandhari nzuri ya kuvutia watalii. Watalii hupenda sana mji wa Moshi kwa sababu ya mlima Kilimanjaro na huduma muhimu kama mahoteli na usafiri.


0 comments:

Popular Posts