Kama kawa leo ni dei nyingine tena mtu wangu tunazisogeza tarehe mwaka ndio uwoo!!! umegeuka Husein Bolt namna unavokimbia fasta unashtuka mtu mzima umeisha alafu hakuna mchongo wamaana ulioupiga town! unajua inakata handasi sana...?
Asa kuna wanangu dizaini walishasanuka huu mwaka unaeza isha bado wako vile vile si wameamuakuji mix mitaani nao wachenji laifu sio kubaki kama mwaka jana si unaelewa zile, basi unaambiwa wana wamejipiga piga wamefungua bonge ya senta apa mjini kati wao ni kuwa pendezesha dada zetu, umenisoma eeh!!?
Asa unaambiwa wana zao siku hizi ni Thailand hadi kule kwa huu!! tang shii maaasta!! uchinani yani, mishe kubwa ikiwa kwanda kukagua mizigo mipya sokoni yani kama ukitaka kupendeza bi'dada we wapandie tu wenetu pale town afu ni very simpo yani bei zao.
Nikaona Zee sio kesi wala kelele kama nitaenda wacheki wnetu nikabariki pale golini si unajua Zee nahudumia bi'mdogo mmoja hapa town asa nikaenda mpendezesha kwanza tukizidi kuchunguzana kama wenyewe wanavyodai huko kwao!. Nikakuta masala wako kama kawa yani mzigo ndio fulu kila kona yani ukitupia jicho kile kizuri Zaidi ya hichi unaambiwa alafu yote praizi ni chipu!! na orijino yenyewe si fua nichuje.
Nikampitisha bi'mdogo awochi mwenyewe huku Zee nikila stori mbili tatu na wanangu pale kawa mzuka sana. Si unajua tena kila kitu kina changamoto zakeasa hizo changamoto ndio Zee nikawa nataka kuzijua ili dei na mimi nikifungua ishu kama hizo mikoani niwe nina kaeksipiriensi kidogo nisije kula losi yakutosha.
Wale wanangu kunipa mwanao darasa huwa hawawazi kabisa ni ile frii hakunaga ada alafu materio ndio yenyewe yani. Si unajua akifanikiwa msela kimefanikiwa kijiwe! iyo ndio rul namba wani yani mwenetu kila kona sambaza huo upendo hapo.
Umeona mwenetu wana si wakaanza kufunguka unaambiw hii bizinesi ina majanga kinoma noma kama huna manoleji unaeza kufa maskini mwenetu. Kuchepuka kwenye hii bizinesini kama kawaida ila ile busara unaeza usichepuke kiivyo si unaujua ule ujana wakwenye friji ule si huu wa majiya moto yani ule unaokimbilia majukuumu hapo mwenetu tiyari unaitwa faza ndio utakuwa mpole.
Asa mwana akanitonya unaambiwa hadi wake za watu wakubwa tu town wanatega kinoma asa Zee nika shangaa kidogo hiyo inakuwaje..? unaambiwa pale si kuna ki rumu chaku testiya pamba asa wale wenyewe wale masukari wakija pale hadi zile za ndani wanazi testi afu wanawauliza wana hapo vipi na fulu mitego si umpatapicha mwenetu!!? dah! ndio Zee nitaziweza izi biznes kweli..?
Wana wanakwambia samutaimu ile kuonesha uko aktivu wana wanawabandulia pale pale unaambiwa yani kesho waje kuungisha biashara tena patamu hapo!. Wakati naendelea bonga soga na wenetu pale bi'mdogo naye ndio akawa amemaliza ishu zake Zee nikawakeshia wenetu chao niwaambia nitarudi suni sisi tukapita hivi.
0 comments:
Post a Comment