Asubuhi nyingine tena Zee ndo nimeamka mtu wangu na hang
over ya hela kama mwanangu Joh makini wa kaskazini, fasta fasta bila kupoteza
hizi sekunde naji flash ile kisela zee lionekane smart sharo si unajua dada zao
tena.
Mjanja wa kitaa ni wakuwapitia pitia alau wawili watatu na utawapataje sasa mwenetu kwa mfano ndo wewe kivipi labda…? Anyway tuachane na
ilo zogo ila zee linamaujanja yakutola wewe lifuate tuu wenyewe wanalitaga
swagga boy.
Ila mwenetu vipi sasa michakato wa kutuia supu kwa mazaa
pale kati ngoja Zee nikajenge mwili siunajua apa ni manyutrienti ndo mpango
mzima babake’. Karibia mezani hapa mwanangu tuzikagulie mdomoni hizi chapatti za
Azam.
Sasa hapo mzuka embu lipange dili hapa tukalichangamkie
chapu chapu kuongeza uchumi wa Tz yetu, naanza kuikatiza mitaa ile kicheki bob kajua
cha saa nne sasa naona nikatize huku uswazi sindio wanakokuita kwa wajanja wa
town.
“Weweee!!! Kuwa makini fala wewe barabara za watu hizi
hangaa shangaa tu!!” tobaa! Zee nikajirusha ile kininja ninja kufuata amri ya
huyu bodaboda asijenigonga na tororoo lake bure, nilikua sijaamini wale wazee
wa kwa mpemba walivyokua wakiwalaumu vijana wa huku uswazi asa leo ndo
nimewajua japo kidogo.
Unajua ni nini Zee nilikua nashangaa..? ni huyu braza men
mmoja apa yupo na sista du! Matata sana wenyewe huko town wanawaita
visuu..unavijua wewe asa visu ni watotoama wachuda wazuri daka iyo toka kwa Zee
ama ticha wako.
Mwanangu unazifahamu zile gari aina ya Alteza..? sasa ndo
huyu braza men amelipaki hapa af kafungua mlango na bonge ya mziki unapiga tena
ule wa Rick Ross mpya mpya hivi. Embu ngoja mwanetu ifanye ukachero
kidogo..Alaa kumbe ichi ni kigrosari cha kishikaji ngoja Zee nijisogeze
nimchekishie huyu mrembo wa braza men siunajua Zee mtu wa mitikasi taaluma
nyingi asi vunga chalii.
Hawa wahudumu wako fasta kinoma yani kuvuta kiti tu uyu hapa “Kaka
nikusaidie kinywaji gani…?” Zee kama niko ndotoni vile sauti nyororo imepenya
kwenye ngoma ya sikio acha Zee nicheze Samba sasa. Siunaona mrembo saivi ni
mida ya kazi naomba nisaidie Juisi baridi tropical siunajua Zee sina undugu na
Bakhresa ila natupia bidhaa zake kinoma noma.
Juisi imeletwa tu Zee nikamtupia Yule mhudumu jicho zuri Zee
kiboko kitu kikatabasamu kwanini na Zee nisitabasamu..? ila huyu namweka akiba
kesho ntarudi tena. Huwa Zee sipendagi usumbufu nikachukua kimeo change nikaanza
peruzi peruzi huu namchabo ule mrembo wa braza men.
Basi unaambiwa demu kamganda mchizi kama gluu zile asogezi
jicho kando kudadeki, Ila Zee nikaona No sweti ngoja nivumilie kisela. Muda wa
kama robo saa hivi ukapita Zee sijaona dalili ila yaliyokuwa yakiendelea hapa
grosari ni fulu bongo movie unaambiwa demu kumbe ni kicheche kimoja kinakaa
nyuma tu ya hapa grosari msela ndo anamaliza nacho mambo yake kimya kimya ila
ni vipi vipi huyu mchizi kuchukua demu karunje kiivyo..? Zee lipo kazini hapa
nazidi kula Info za huyu mrembo wa braza men toka kwa msela mmoja hapa grosari,
usiulize nimejuana naye kivipi we jua Zee ndo ticha wako mtu wangu.
Kama mazabe Yule tozi akanynyuka kwenda wapi sijui Zee ndo
nikaona yesi hi ndo chance waropa wanavyoitaga ile nataka kusimama tu mrembo
akaniwahi huyoo akatoka kwenye gari kacheki cheki akapiga simu sijui alikuwa
anabonga nini Zee nikatulia kwanza Yule mrembo kumaliza tu kuongea akarudi
kwenye gari akatulia. Braza men akarudi kama dakika moja badae nikajua kumbe
msela alikuwa ameenda msalani
Demu kampokea kwa mbwembwe kama kawa wakaendeleza mchezo wao
mchana mchana. Dakika kama tano mbele nikaona demu kama kashituka hivi na msela
naye ameshituka Zee nikajiuliza kulikoni pale kucheki kaunta kumbe kuna wasela
wengine kama wanne hivi wamekuja pale wakaagiza vinywaji nao wakatulia dakika
kama mbili tatu mmoja wao akasimama pale akanyooshea mkono lile Alteza la Braza
men
“Ndo huyu huwa anamchukua shemu broo!!” nikashituka kidogo
vipi hapa fumanizi nini ama ndo sinema linaendelea “Huyoo huyooo!! huyoo!!”
wasela hao kwenye gari la tozi demu naye akaanza kama kulia anaomba msamaha
tena analia kabsa “mme wangu nisamehe ni amenitongoza tu” Braza men apo ni
anatetemeka tena si kitoto ile kkubwa kabsa mwenetu.
Ikawa bonge la picha raia nao wakaanza leta wingu pale si
unajua uswazi tena Zee nimekuwa mpole apa natafakari hau kamu!! Si nimepewa
stori hapa huyu ni bonge la kicheche!!? Asa huyu msela kaniingiza Zee chakike
leo nkamgeukia nianze kummaindi vipi mwenetu au ulitaka na mimi nifumaniwe nini…?
Msela akaniambia kuwa mpole kaka huu ni mchezo tu pale
hakuna cha mume wala mke watu wako kazini pale .. Nkaona huyu naye ananiletea
stori za Abunuasi hapa Zee nikarudisha macho kwenye fumanizi nikakuta Braza men
keshahukumiwa siku mingi ni anahesabu vitita tu pale “Bado bado hazijafika laki
tano”
Ndo nilichokisikia akisema mmoja wao pale Duh!! Braza men
kapigwa parefu hivi. Ile kutoa tu wakamruhusu naye mbio kwenye gari lake
mwendoo!!
“Kaka umeonazengwe hilo..?” ndo swali la msela baada ya
braza men kusepa na Alteza lake demu akajifuta futa pale huku anabonge la
tabasamu kwa wale masela, duh!! Nimeliona mwenetu kumbe si kila fumanizi ni
laiv mengine bongo movie tu!!
Zee nikamchabo Yule demu hadi hamu ikapotea kabisa kwa Yule mhudumu
nisijikutana na zengwe la braza men buree!!...ila Zee si ndiyo ticha wako huyu ngoja
nitampitisha chocho zetu zile pale town adate mwenyewe ‘wani dei!!’
Zee ngoja nikapige lunch tusomane baadae mtu wangu!!
0 comments:
Post a Comment