KUTOKA KIJIWENI__UNAAMBIWA HUKU NI MREMBO ATOSWAA NA YEYE ANAJITOSA ZAIDI__BOFYA HAPA KUSOMA KISA KIZIMAA!
NA MWANA KIJIWE
Leo habari zimekaaje wanangu!..? mimi ni fresh sana ila dizaini leo mishe zilikuwa nyingi sana yani unaambiwa mtu mzima nilikuwa nafanya michakato na wanangu wa pande za MJ si unapajua wewe basi Zee ndo nilikuwa na krieti mavitu Fulani.
Hayo tuyaache kwanza maana nitakuja kutupia ma nyuzi ya mchongo mzima ulivyokuwa pale kati zile za yo!! yoh!! yo!! Zee si ninaziweza..?. Basi tukatoka pale kufanya yetu kwa vile nilkuwa na mwanangu mmoja wa ukweli tukaona yes! ngoja tukatembelee vijiwe vya masala wa mitaa ile tuone inakuwa ni vipi michakato kitaa wana tulengeshane maishuu.
Wewe si ulishazisikiaga zile stori za watoto wakike kutoswa na wana..? sasa unaambiwa huku ndio swagga sasa yani watoto wakiume wananata kwa wachuchu hawana taimu wenyewe uzungu mwingi Zee nikawashangaa wana vipi ni mpaka watoto wawatongoze nini..? basi nikikaa pande hizi Zee nitakuwa mchepukaji sana mwanangu mwenyewe.
Kutaka kujua sasa dada zao wanachukuliaje ishu za kufungiwa vioo na maboyz wa huku nikampandia angani mwanangu wa kipande kile.."Oya mishe ni gani? Zee nipo kitaa hapa wapi wewe tuchekiane..?" mwana akaniteli "dah!! ni mzuka baaria wangu ila nipo mbali na hozii hapa ila sio kesi we nipooze pale skani kwetu si unapakumbuka pale wana kibao wako" Zee nikaona ni gudi tu ngoja nimvutie taimu huku napiga soga mbili tatu na wadau.
Fasta nikavuta atua mbili tatu na mwanangu yule fasta tukaibuka kistone kwa mchizi hai mbili tatu na wadau ikawo mzuka tulikumbukana pale na wale washikaji tokea pande za kaskazini watani wa Zee wale. Mwana alikuwa kajijenga si mchezo bonge la gereji la mandinga ya maana unaambiwa na kimini supa maketi pembeni ile kishua Zaidi
Akaja motto mmoja mzuri ile kinoma Zee nikaona wana nini ile salamu tu alafu bati yani unaambiwa ni buyu no stori mingi dah!! na mimi nikasema ngoja ninate kwanza ila kama kila kita kingekuwa hivi walahi tungekuwa tunabakwa masala.
Si unanijua tena Zee mtu wa swagga nikataka kujua wai wana wanakula bati namna hii mwana mmoja mchaga yule naona si ndio akaanza funguka ni unaambiwa ile mitaa mwanzo wana walikuwa gudi sana zile tongoza tongoza zilikuwa kama jadi ila sasa awo watoto wakike kunata ndio sana alafu dizaini wakawa wanapitiwa na machizi wa mitaa ya jirani.
Si ndio wakasema hiwezekani basi na wao wakapitisha azimio unaambiwa ni bati ama buyu mwanzo mwisho akuna zile shobo wala nini, wenyewe wakajirudi si akuna tena zile kusifiwa ila unaambiwa ndio zile tu leti wana wameshaamua kitambo. Mpaka leo yani wana ni mwaka kama wa tano hizi akuna shobo kabisa madenti uunaambiwa ni wanataka hadi samutaimu kulia yani ila ndio msimamo yani ukawa awaoni ndani hapo.
Tunapiga soga pale mwana ndio na yeye akarudi pale skani, kweli watu wanabadilika mwenetu unaambiwa mwanangu huyu alikuwa ni mtu wa totozi Zee naigiza ila nau deizi ndio kawa kadinali kichizi yani, chunguza chnguza si ndio wana wakanitonya stori moja kuhusu mchizi unaambiwa alikuwa asababishe mauaji laivu laivu ni denti mmoko anakaa kama hatua ishirini hivi tokea pale mwana akanionyesha ile kwa kidole tu ni bonge ya bangaluoo yani
Unaambiwa alidata na mwana kinoma na ukimcheki mwana ni tolu kama Zee hapa ila yeye kajaa jaa na mkoko anao ule wa range sport vogi mwana ni faru kinoma yani unaambiwa tokea babu zake wote ni ma richi pipo wenyewe. Sasa denti kudata na mtasha mwenyewe mwana wala hata zile kushoo interesti ni ziro tu! hana taimu yani unaambiwa denti akajipa hopu ila dei ya dei mhuni wangu unaambiwa kashajitupia vitu vyake akamchana demu laivu laivu yeye anaga zile interesti kabisa yani ni anajisumbua tu bonge la toso yani.
demu akaona ataa akaamua kulia tu pale fuata ana wa mchizi ila wapi mwana abadiliki msimamo ni shida huo. denti unaambiwa akaona isiwe tabu sana unaambiwa eti akaona yeye katoswa basi bora na yeye ajitose Zaidi si akajinywea sumu, ila ile kama zali vitu vimemzidi ile kuwa nalia kitandani wazee ndio wakashituka kunani tena ni ile fasta hospito.
Homu wakakuta bonge ya leta yenye mkanda mzima wa kutaka kujitosa mwenyewe unaambiwa wazee wakamfuata msela amkubalie mwanao kwanza ni msela akawa mdogo kama piritoni ile hau kamzi nisababishe mtu ajitoe uhai kisa mimi..? ni bahati tu mwana ni mtu mmoja mwelewa akaona isiwe tabu ngoja ni shoo lavu.
Fasta mwana akadandia ndinga lake hadi hospito kumcheki denti na matunda matunda si unajua za hospito zilivyo basi ndio mwana naambiwa hapa yupo michakatoni atuachie sisi ubachela wetu.
kwa nini Zee nisimpe mwenetu mashavu..? au unaniambiaje mtu wangu mwenyewe yah!! ivyo ivyo yani acha tutoe sapoti kwa mwenetu.
yani ni toswaa ujitose!! badae mtu wangu wanguvu!
0 comments:
Post a Comment