background img

The New Stuff

KUTOKA MITAMBONI NI STORI YAKUSIKITISHAAA!!!__BINTI WA CHUO KIKUU MAARUFU HAPA NCHINI AFUNGUKA KUHUSU PICHA ZAKE ZA UTUPU__BOFYA HAPA KUJUA KASEMA NINI



NA MWANA KIJIWE
"Ilikuwa ni siku ya ijumaa jioni nikiwa hosteli...(anatulia kidogo akionekana mwenye masikitiko mengi) ile siku sitaweza kuisahau kirahisi maishani mwangu hapa duniani." hii ndiyo kauli aliyoitoa mwanadada huyu ambaye kwa kweli ukimuangalia tu hautasita kuuridhisha mwili na akili yako kuwa kweli huyu ni mmoja wa mabinti warembo Tanzania.

Swali langu la msingi lilikuwa ni kutaka kujua kulikoni akapiga picha za aibu na kuziweka mtandaoni..? swali lililoonekana kumfedhehesha sana binti huyo na kumweka katika hali ya majuto lakini wahenga walishasema mjuto ni mjukuu.

"Unajua kaka sikuwahi kufikiria kupiga picha za namna ile kwenye maisha yangu na wala sitakaa nipige picha za mtindo huo" kauli hii unaweza ukaichukua kama ilivyo na kuiona pengine ni kauli ya mtu asiyejua anachokisema au labda karopoka tu.
 Wala sitakaa nipige picha za mtindo huo...? ndiyo swali lililonifanya intake kujua Zaidi undani wa picha za dada huyu ambazo zimekuwa gumzo kubwa kwenye mtandao mbalimbali hadi kufikia hatua ya kutengwa na ndugu zake mwenyewe ama kweli hili ni pigo kubwa kwake.

lakini kama si yeye ni nani kwenye picha tunazoziona mitandaoni..? je ni editing au ni kitu gani..? ndiyo maswali niliyokuwa nayo kichwan nikaona sasa ni muda wakumuuliza mhusika mwenyewe
"Kweli kwenye picha ni mimi mwenyewe wala siyo editing"
"sasa kama ni wewe kivipi useme hujawahi na wala hutawahi kupiga picha za utupu ilihali tayari unakiri kuwa kwenye picha ni wewe wala siyo mtu mwingine.?"

swali langu hilo ndilo lililomfanya binti huyu anielezee kisa kizima kilivyokuwa
"..Ilikuwa ni siku ya ijumaa jioni nikiwa hosteli alikuja rafki yangu mmoja wakike na kuniomba nimsindikize maeneo ya mbezi kwa rafiki yake wa kiume...kwa kuwa alikuwa ni rafiki yangu kipenzi sikuwa na sababu ya kukataa kumsindikiza ukizingatia aliniambia anaogopa kurudi peke yake hosteli. Nilimwambia anisubir nijiandae nilipomaliza alinisifia sana kuwa nimependeza sana nisije mtamaniisha shemu wangu, tulicheka kwani utani ilikuwa kawaida yetu. kwa vile mwenzangu alikuwa ana gari ilikuwa rahisi kwenye suala la usafiri mwendo wa dakika 30 na foleni ya hapa na pale tukawa tumefika mbezi beach maeneo aliyokuwa akiishi huyo boyfriend wa rafiki yangu.

Tulipoingia ndani nilishituka kidogo kwani kulikuwa na  watu wengine takribani ishirini  wanaume na wanawake nilipomuuliza yule rafiki yangu aliniambia kuwa likuwa ni part ya boyfriend wake. Nilimuuliza kwa nini hakuniambia toka mwanzo ila alijitetea kuwa kama angeniambia ningemchukulia shemu wangu zawadi na pengine ningeingilia uhusiano wao..rafiki yangu huyu huwa ana wivu sana ila nilishamzoea nikaona kawaida.

Baada yakusalimiana na watu kadhaa nilienda kum-wish shemu wangu happy birthday. Muda ulikuwa ukienda mbio kweli tayari ilikuwa saa mbili usiku tunacheza mziki ndipo akaja kijana mmoja kuniomba kampani yangu nilimkubalia tukawa tunacheza wote ikizingatiwa nilikuwa tayari pombe imeanza kuni-control. Tulicheza muda mrefu sana huku akinisifia kuwa najua kucheza na pombe ndio ilikuwa imeshanichukua kabisa nilikumbuka kunakurudi hosteli. Nilimwambia yule mwanaume lakini aliniamba kuwa nisiwe na hofu kwani atanipeleka nilimwambia sawa ila acha mimi nirudi kwani nipo na rafiki yangu na yeye anausafiri ndio tuliokuja nao..aliniachia nilipoenda kumwangalia rafiki yangu naye alikuwa kasha lewa hivyo asingeweza kuendesha gari.

Kwa vile nilikuwa natakaka kurudi hosteli usiku ule ule nilimkumbuka yule kaka na kurudi alipokuwa, nilimkuta pale pale anaangalia watu wanavyocheza nilimuomba anirudishe hostel alikubali ila aliniomba na mimi tucheze tena kidogo. Nilikubali kucheza nae tena kwavile nilitaka kurudi hostel.
Tulitoka pale nyumbani kwa shemu wangu na kuwaaga walokuwa pale safari ikaanza kurudi hostel, tukiwa njiani yule kaka alinipa bia nyingine ya kopo wakati naendelea kuinywa nilizidiwa nayo nikawa sijitambui vizuri. Yule kaka alinifikisha hadi hosteli ila tulikuta geti tayari limeshafungwa Alinishauri nikalale kwake kesho atanirudisha asubuhi nilikubali kwa vile sikuwa na jinsi nyingine tulifika kwake na mimi nilikuwa nimechoka hivyo nililala moja kwa moja

Asubuhi alinirudisha hosteli..Kwa kweli nilimshangaa sana yule kaka kwani hakunifanyia chochote kibaya usiku ule. Nilitokea kumpenda na aliponitongoza sikukataa kwani nilimuona ni mtu mwaminifu.
Tulidumu naye kwa mda mrefu kidogo kwenye mahusiano ila siku moja aliniambia kitu kilichonifanya nikavunja naye mahusiano. Aliniambia tufanye mapenzi kinyume na maumbile nilishangaa na kukataa kabisa, alizidi nishawishi sana alipoona nimegoma kabsa na kuvunja uhusiano naye alinipigia simu siku mojana kuniambia niingie FB (facebook) kuna picha kani 'tag' nilipuuza nikaendelea na shuhuli zangu badae dada yangu alinipigia simu na kuniuliza toka lni nimekuwa mcheza porn (filamu za uchi) alinishangaza sana ila aliniambia ameikuta kwenye profile (ukurasa) yangu Fb nilishituka na kuamua kuingia mwenyewe ndipo nilipokuta picha hizo za utupu ambazo nilikumbuka ni siku ile ya party ya boyfriend wa rafiki angu tena nyumbani kwa yule kaka nililia sana siku hiyo

Nilipomtafuta yule kaka hakupatikana tena na tayari picha hizo zilisambaa blog nyingi sana hadi chuoni, niliishi kwa mashaka sana chuoni. Nyumbani nako walinipigia simu kutaka nisirudi kabisa likizo wala nyumbani kwani nimewatia aibu kubwa..." Huku akilia hakuweza kuendelea kunipa simulizi hiyo iliyonifanya niinamishe kchwa chini huku nikimuonea huruma.

Hapo ndipo nikakumbuka na wale dada zangu wengine vyuoni wanaopenda kujirusha yasje watokea kama ya mwenzao.

0 comments:

Popular Posts