Kwa muda wa takribani wiki mbili sasa kumekuwa na fununu za kutaka kuanyika maandamano yasiyo na kikomo nchini kushinikiza bunge maalumu la katiba kusitishwa.
Mjini Arusha nako hali imeonekana kuwa ya wasiwasi huku wanachama na wapenzi wa chama cha CHADEMA maeneo ya Arusha na majirani zake kiwemo mji wa Moshi wamekuwa wakiwasiliana kwa njia mbali mbali mitandaoni kuelekezana na kuhimizana kuhusu maandamano hayo yasiyo rasmi.
Ikikumbukwa kuwa Chadema ni moja ya vyama vinavyounda UKAWA ambao walisusia bunge maalumu la katiba sasa wanadaiwa kutaka kufanya maandamano hayo, huku mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe akiwa ameitwa kuhojiwa na jeshi la polisi
0 comments:
Post a Comment