background img

The New Stuff

TETESI ZA MHUSIKA___MWIMBAJI WA INJILI FROLA MBASHA AFUNGUKA "NINA MIMBA YA MBASHA"


KUTOKA MTANDAONI
Akiwa katika kipindi kigumu mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Frola mbasha ameweka mambo yake bayana ikiwa ni mpango wakupingana na habari zinazozagaa mitaani kuwa amekuwa akifanya maba ambayo ni kinyume namaagizo ya mwenyezi Mungu.

Akikanusha tuhuma mbali mbali juu yake mwanamama Frola Mbasha alisisitiza kwa kusema kwanza hana uhusiano na mchungaji Gwajima kama inavyoripotiwa mitandaoni kwani Gwajima ni mtumishi wa Mungu pia ni mjomba kwake hivyo hawezi kuwa na mahusiano na ndugu yake.

Pia msanii huyo alienda mbali kwa kuweka wazi kuwa kwa sasa ni mjamzito na ujauzito huo si wa mtu mwingine bali mumewe Emmanueli Mbasha ambaye kwa sasa anakabiliwa na kesi mahakamani, kwenda mbali Zaidi mwanamama Frola alisisitiza kuwa bado anampenda mume wake huyo japo wana misukosuko katika ndoa yao na hapendi kuiweka kwenye vyombo vya habari kwani kufanya hivyo ni kumkosea heshima mumewehuyo.

0 comments:

Popular Posts