NA MWANA KIJIWE
Adjee!! mwenetu mwenyewe wa ukweli!? pande hizo ni vipi, kumejaa Amani siyo? apo yesi pisi endi lavu si ndiyo mpango mzima mwenetu. Ujue bila iyo kitu hapa duniani kungekua kumeshaangamiaga kitambo ana mwenetu wewe angalia tu lile tukio la vita vya dunia unaambiwa lilikuwa na parti mbili yani wani na tu! kama muvi vile ni shyiiigidi shida mwenetu.
Asa kwa nini tusisambaze upendo huku kitaani na nasikia siku hzi wakubwa wa dunia wamesema eti hapa homu bongo demokrasia imeshuka ujue hizi ndio nyakati za mwisho hivyo kwaiyo na wewe mwenetu sambaza upendo kitaa chenu hicho.Ila ujjue ni nini leo sitaongelea ishu hizo sana naona tuishiehaponikupeleke kwenya mada yetu ya leo, yani kama ni barua kipindi kile tunasoma elimu ya UPE basi ningeanza na neon kichwa cha habari hapo juu chahusika hahahaha!! ila ujue yule ticha wetu alikuwaga mtata sasa tukawa tunaandikaga hivihusika na kichwacha habari hapo juu si umeonatofauti hapo mwenetu..? au ujazisoma!! hahaha!! ila wewe mjanja najua utarudia kuzisoma hizo sentensi mbili huku Zee nikizidi kukata mbuga!
Asa leo nilikuwa kijiweni bhana unaambiwa hiidunia sam taimu kuna watuwamependelewa miili mizuri au sijui inategemea na maeneo eti ee!? maana leo nipo kijiwe Fulani ushuani ndio naona ma vituzi nakumbuka mwenetu wa pale kati anaitaga mizigo hahaha!! ujue kuna wana ni ediktedi kabisa yani na hiyo mizigoasa wakija huku dah! ndiyo zile kesi za ubakaji hazitaishaga kabisa yani. Ujue niliyoyaona huku hayafai kusimula unatakiwa uje mwenyewe uyaone aisee maana dah! kuna mambo kama ugaibuni.
Nikasema ngoja nile stori mbili tatu na wana wa huu mtaa huyoooo hadi kijiwe cha wenetu ma raida si umenielewa hapo yesi! wale wanaowapeleka kule siti senta wakubwa wa huku. kwanza wao wenyewe ni tofauti sana na wale niliowazoeaga mitaa Fulani ujue ni changamoto wenetupande zenu huku wanapiga unifomu kabisa yanii wako smati kinoma si unajua kwa wazito huku, lakini embu ngja kwa nini na nyie wanangu wa uswazi msiige wenzenu wa huku? mjue sam taimu mnazingua sana ndiyoo! Zee si ndio ticha wako acha nikutichi sasa mwenetu hata ukimaindi haina noma ila utaelewa tu!!
Ayo tuyaache maana ujue mwenetu nakuwaga na hasira yani au wewe unaonaje hizi mishe unapakia tukutuku afu raida mchafu kinoma yani koti unakuta kalitupa hata wiki hakuna maji wala nini, mimi huwa sivungagi nakuchana mazima mwenetu unazingua eee! kwani ni uwongo mwenetu?. Hapa hiyo ndiyo nilianza nayo kama mada unaambiwa hawa ma raida wa huku wenyewe wanakwambia wanakerwa sana na tabia hiyo ya wenzao wa pande zingine "Braza asikwambie mtu kila kazi nahitaji unadhifu kama haupo sopu sopu hata kama unapiga kazi kama bosi gani sijui huko town utaonekana choko tu hapa mjini!" aliniambia mwana mmoja aliyeonekana ni muongeaji sana hapa kijiwe si unajua ao hawa jamaa ni maneno mengi ila mi mwenyewe nimem'maso mwenetu vip wewe?
Asa nikataka kujua ishu za kupiga vya ukucha kabla ya kuraidi mzigo mzima "mjomba kama unataka tukutimue hapa kituoni kwetu yani huwe na hizo tabia tu! yani hapa ulevi ni mwiko broo! na tushawatimua wana kibao tu sahivi wapo huko uswahilini huko" aliniambiammoja wa maraida ambaye kwa kumcheki tu nikajua mtu mzima hapa natakiwa kutoa shikamoo ghafla mwingine akadakia ada kwa mbele "Na wengine washafarii kamanda angu" si unajua zao hawa makamanda zangu wewe ukitaka info za town wachungulie hao yani.
Wakati tunapiga mastori pale akapita raida mmoja kabeba bonge yya toto unaambiwa imemkumbatia ile ipasavyo akapiga honi tu pale kuashiria uwepo wake hapa kijiweni huyooo akaendelea kulisebenza goma! tena si mwendo wa kitoto ujue apo nikapata kamadachaku introdjuzi papuu!! mwana ni raida wa pande hizi naye ama mbona yupo mwendo wa faru kimtindo? "Yule mwenetu san hapa kituo tunamwitaga mwiba yani ni mtu wa totozi sana yule we mwenyewe si umeona toto lile asa ndio wateja wake sana sana" Ujue truu! mwana kapita na msumari hatari sana hapa nikasema ngoja nimwulizie Zaidi huyu mwana ujue mi huwa nasikia sana washua wakilalamika watoto wao wanaharibiwa na hawa maraida zetu asa huwa na watetea kinoma ila kumbe sam taimu nazinguaga ee!?
Si umeona ile spidi ni unaambiwa pale yule mototo basi atakuwa analalamika ile yakubembeleza tu si unajua zile za Jamanii we kaka uhuu!! taratibu bhasi!! hizo hizo na mikumbatio yakutosha asa mwana yeye anafurahia sana hizo mambo za dereza boda boda nipelekeeh pole pole!! yeye olaa ndio anadataga ase huyu raia wa ajabu kweli yani mwenetu ila unaambiwa wanampendaga kinoma yani watoto wa kike siyo mchezo mwenetu ni mtani kinoma unaambiwa.
Ile tunaendelea kupiga soga pale mchizi naye huyoo hata asemwi akaja pale kijiwe fulu uchangamfu akatembeza gweraa kwa wana naye akapozi tuendeleze libeneke pale kijiwe nikasema yesi ngoja anipe michongo miwili mitatu hapa town inakuaje!.
Hii mwenetu nitakupa badae stori za huyu mwenetu si unajua maraida ni mwendo wa kuraidi tu asa ngoja na mimi ni raidikimtindo mwenetu!.
0 comments:
Post a Comment