NA MWANA KIJIWE
Habari za siku kama siksi mwenetu mwenyewe!!! ujue mimi ninakuaprishieti sana mwenetu..? wewe ujajua kwa nini tu bado..Aaah! usiniangushe mwanaobana si kwasababu umekuwa mzalendo wa kijiwe chetu ujue kuna wana samu taimu kama wanazinguaga vile wakisikia kamanda wao kasafiriyani ndio mwisho wakuzuka kijiweni dah!! ujue siyo ishu gudi kabisa kwani wewe mwenetu unasemaje..? Ila kweli muda mwingine inabidi wana wakigomee kijiwe sasa kama hakuna cha maana kijiweni si bora watu wakajimixi ili mradi kupata kitu kwa maisha ujue gudi laifu si kirahisi mwenetu!.
Ila hayo tuyaache ujue mwnao Zee nilikua nimesafiri kidogo ndio maana ukaona sizami kijiweni ila si mzuka wala nini yani nimesepa ile ki bushi loya hakuna kumsanua raiya ila ujue wanga wengi mwenetu so samu taimu inabidi tu aplayi ujangili kidogo...Vipi mbona umeshituka mwenetu..ndiyoo ujangili kidogo ila usije mtonya mkubwa ukanigeuza msosi wa wadosi buree! na nakujua wewe mwenetu huwezi nichomeshea utambi.
Asa mwenetu tuachane na mboyoyo nyingi kwanza umesoma ilo li hedingi apo juu, ilo ilo mbona dizaini unataka lirudia tenamwenetu.. ulilisoma bana ndio maana uka kliki kupata ma infomesheni Zaidi umenisoma ee!?. Asa nilikua kwenye mishe zangu mjini kule wenyewe wanavyokuitaga si kule daresalamu babu!! yule msanii aliimbaje tena sijui kama nitapatia ila huyo huyo "Ulikuja kimwana,msichana tena hujui kuchuna ee," wenyewe mnamwitaga Ali Kiba ila kuna kijiwe nilikuta wanamwita Ali kuiba asa sijui walikuwa na mchongo gani na huyo mwana akazingua ila ayo tupa kule mwenetu. Kuna wenetu wapo pande za Rau pale Mo Town wenyewe wanajiitaga Rau Unit asa wana ngoma lao moja linaitwa Na2pa kule embu fanya na wewe kutupa kule afu tuone itakuwaje mwenetu, Ujawafahamu awa jamaa embu fanya kuwa gugo utaona vitu vyao tu ila awo nao tuwatupe kule au unaniambiaje mwenetu..?
Basi nikiwa jijini si nikasema embu ngoja nizame vijiweni kucheki na wana si unanijua ticha wako sikawizagi mishe mi kokote naibuka tu mbona mdogo mdogo nikajisogeza hadi kituoni ilikuwa ni Moroko pale kama sikosei chapu nikadanda DSM za Mbagala rangi tatu wenyewe wanakuitaga hivyo huyooo hadi kona ya taifa nikasema Kondo embu niache kwanza hapo nikawape hala wanangu wa Chang'ombe chapu!! na yeye akanisikiliza tukapatana manauli mwanao huyoo nikaanza kuzivuta kwelekea Tcc Club! mbona umeshituka mwenetu umepata lipicha kamili siyo ujue mwanao nina makoneksheni woldi waidi aise.
Kwani kilonga kazi yake I nini mwenetu nikaona isiwe kesi nikawapandia wanangu hewani capu "Ouya mi nipo hapa Tcc napiga raundi mbili tatu kama vipi ibukeni chapu mapemaa" iyo unaivuta kimadaha kwanza huku natupia vitu wan nao hao! na yule mwimbaji wa ugali anaitwaga nani vile achana na yule wa si unakataa ugali awo walifanya kuzinga tu yule mwenyewe yule ogii yani ekheeee Sa' Kiblaa juma Nature.
Anapenda kubonga huyoo we ukitaka ku pruvu mi rongu' ibuka tu Tcc pale utamkuta yuko zake kwenye puli tebo yeye ni kuongea tu! ila na yeye tupa kule tusonge zetu na wana si unajuaata mimi staa bana au unasemaje mwenetu mwenyewe dizaini kama nazingua ee..? wewe tuliza boli mi naona wewe ndio unaanza zingua eti mara Ooh!! Zee kichwa cha habari akiendani na habari apa ni blaablaa tu!! embu vunga tu mwenetu au kama vipi tembea si mimi mwanao azi longi wewe ni mwanangu mimi nakuchana tu!
Asa tuendelee mwenetu si uyu mchizi alitaka nitoa kwenye mudi aisee astukapiga tori nyingi sana pale tena nyingi kinoma na fulu mikakati ujue mwaka ndio unisha hivyo afu hata la maana hakuna muda ukazidi kutembea huku mambo yakubonga ndio yanazidi ila si unajua mwanao ni mtu wa ratiba ama taimu tebo kwa kimombo nikaona jogaa lisije wikw afu nipo hapa Chang'ombe hata cha mbuzi sijafika kulaleki nikaagana na wana pale wakaniambia nivunge wananirudisha maskani nikawambia wana acha nikapkie dala dala nipate mikasa wenetu wakanielewa ila wakanisisitiza kinoma nisiache watembelea nikawaambia aina dazi hiyo.
Asa hapa ndio kiini cha ishu yetu yaleo hapo juu ilikuwa ni introdaksheni tu wanangu, nikadandia ndinga za Mbagala Kawe si nikakosa siti ya kukaa nifanyaje tena duh!! ikabidi kusimama tu wenetu ndinga likaendeleza zoezi la kuitafuta hiyo Kawe fulu makeke yote yani huku raia wanazidi kupanda tu unashangaa mwenetu unaambiwa bongo dala dala haijai abiria bali wanakosa tu pakukaa iyo ni noma aisee.
Ghafla akapanda mwana mmoja yuko tungi balaa yani Zee nikamsandia kuwa mwana yuko misumari nikaamishia waleti yangu mfuko wa mbele si unawajua hawa hawakawii kuliza mtu mzima safari ikaendelea asa mwana akawa amesimama karibu na bi'dada mmoja kifupi ni mashalah kweli kweli yani fulu mpododo kwa nyuma nini na dera lake si unawajua tena watoto wa uswazi walivyo mzee asa mvutie picha huyu sasa bebi fesi ya ukweli mlev si akakosa uvumilivu mwenetu akaanza mubambia sista du! wawatu
Sista du akamshitukia mara ya kwanza akamwambia ile ya chini chini si unjua tena ni dizaini kama zali flani "acha nishika shika" Ila Zee niliisiia iyo nikavunga huku naendelea somea dazi mchezo wa mwenetu huyo ghafla tena huyoo kabambia mzigo safari hii kafanya ku pampu kabisa kama raundi sita hivi mkono juu ya chuma za stafu keria mwenyewe kajikunja kinoma noma. Si ndio sista du akahisi kama kila mtu kaona mchezo kumbe wapi ni Zee tu nilikuwa nakula hii pono muvi ya aina yake kwa nini asimwatuke huko "WEWE BABA JIHESHIMU ETI, UNANIBAMBIA BAMBIA UNANITAKAA!!! MI MKE WA MWANAUME KAMA WEWEETI ALAA!!! DUME ZIMA HOVYOOO!!!" Kila mtu ndani ya gari mdomo wazi hoooo!! wakahisi kama sista du kapanda maruwani vile kumbe walaa unaambiwa mchizi akawa kama piritoni yani mdogooo kanywea kinoma noma si ndio yule dada akapata mwanya wakumuunguzia mwenetu Zaidi akaanza toa mkanda mzima dah!! Ujue nilitamai kuangua bonge ya kicheko ila nkajishtukia mwenyewe yani
Sista du!! akatupa kashifa za kutosha kwa mchizi Zee nikajaribu msaminisha Zaidi ila nikaona huyu mwana alizingua toka long taimu ujue kwanza alikuwa ananinyima furusa yakuukagua mzigo vizuri afu alichoma kila kitu hadi nikashindwa gongea namba kulaleki mwana alivyoona kimenuka aneza angushiwa kipigo mule mule kwenye ndinga akavumilia kama vituo viwili akashuka zake.
Yule sista du! si akanisogelea Zaidi mwanao nikasema yesi ila kwa alivyomchomea mwana at kuongea nay tu si aneza leta izenguo huyu ila mi si ndio ticha wako nikicheki kakuvalia dera la njano afu Zee nimetupia tisheti yangu ile ya njano nkasema yesingoja nichokoze mzigo si nikaingia na swaga yangu ya "sare sare mauwa asiyejua kuchagua tatizo lake ni ulevi" si unakajua ako ka uwimbo asa nikakidondosha mwanao hapa kwa nini sista du!! asibaki kukenua tu meno. Hapo hapo nikapigilia misumari ya kutosha kitu kikaitika chapu!!.
Mwenetu tusomane badae naona hapa kama net mizinguo ntakuletea simulizi Zaidi za hapa jijini
0 comments:
Post a Comment