background img

The New Stuff

KUTOKA KIJIWENI UNAAMBIWA NI HATARI HATARINI__DALALI KWA NAMBA ZANGU NIKODISHIE CHUMBA ILA UNYUMBA STOP!!!


NA MWANA KIJIWE
Adjee adjee wanangu wenyewe humu kijiweni dah!! Mwanao nimekuwa taiti kimtindo ila si unajua zile za motto wa kiume lazima kuchakarika kila pande siyo kuuweka tu hapa kijiweni afu mwisho wa miaka mwanao yule sani mwenyewe anakuja kuuliza faza vipi mbona hata kiwanja huna ujanani ulikuwa na mishe gani aisee!! ujue ni noma sana ilo mwanangu!

Asa mwanao Zee nimeligundua ilo kitambo sana nikaona ngoja nikacheze dili za mingo ndefu ndefu ila si unajuawenyewe wanasemaga laifu izi noti e rihaso it e pafomansi saasa kama ni ivyo kwanini niuweke skani kila dei mwenetu!?

Chapu chapu nikajitafutia zile koneksheni za mjini si unajua kila ishu siku hizi ni koneksheni tu babulai! asa nikajichanganya katikati ya msitu wa magorofa unaambiwa mwenyewe huyo nikatokea kwa washua fasta nikasomeshwa dili mbii tatu za kupiga hapa tauni niweze muvuzisha laifu mwenetu bila ubishi nikakomaa tu kwani siku hizi jobu si kuandika tu makaratasi kadhaa unapewa bingo lako unaambiwa mtu mzima nimeandika kinoma noma kisa mtonyo tu kulaleki ujue nimekumbuka adi laifu la bushi kule ningekuwa nimepiga jembe kadhaa chini afu naisikilizia tu mvua ifanye mambo sasa hapa ni kusali umeme uzingue tu kulaleki.

Ila tuachane na haya yaliyonikuta mwanao huko kwa wadosi nikurudishe kwenye mkasa ulionifanya nijiajiri kuandika mweneyewe hapa. Jana si nilikua mitaa flani nimeuweka kijiweni na wanangu wawili watatu tunakula soga kama kawaida si unajua hii nchi ya Amani mwenetu ingekua ni huko Nigeria tungewaogopa Boko Haram si unawajua hao? Ekhee hao hao mwenetu hatari sana hao.

Sasa katika stori mbili tatu akaibuka kimwana mmoja pale kijiwe anaulizia dalali si mwenetu mmoja ni dalali pale naona atakua aliambiwa aje kutuuliza ili apate mahitaji yake, Si unajua wakora na macho yao asa wakabaki kunata kwa motto adi stor zikapotea kabisa ila si masihara motto ni pini huyo Atari sana s unajua watoto wa vyuo ndio wamefungua vyuo sasa ile kutafuta makazi lazima waibuke kwa ma broka wenyewe ama nimekosea mwenetu basi ma mido men apo je?? una neno tena mwenetu? basi kaushia ilo kwa leo si unajua mwanao ninachapiaga mene taimz

Mwana akanyanyuka na motto kwenda kando kujadili mchongo wao wakamalizana kwa namba za simu mwana huyo akarudi kijiwe motto akapita kutoa shukrani afu akajitelezesha zake, ujue ni sista du! wachache wanaoweza kutoa shukrani kwa masala waliojikalia kalia tu bila plan kwa kuwaangalia mara moja ila wanakoseaga sana watu wanasizi mchana afu naiti ndio wana wabeba kwenda hoteli kubanjuka ujue rispekti kitu muhimu sana

Ila ayo tuyaache mwana ile kurudi kijiwe akatupa huo mchongo wa kutafuta dabo rumu mitaa ya katikati pale huyu sista du!anatafuta mjengo mbona fasta raia wakaanza panda hewani kuulizia kwa wenetu wengine fasta kama nusu saa hivi mzigo ukapatiana ila sasa kila mtu anataka ampeleke motto mzuri ii ageuze mzgo wake umepasoma hapo!!? yani huku raia wanakutafutia chumba na unyumba kabisa dah!! huku hatari sana yani ukisikia mwana anamichepuko kumi huku usishituke kabisa na wake za watu wana maindi kuwepo hawa masista du wa vyuo huku we achaga kabisa.

Zee nikasomea gepu nikaona hapa magumashi tu mbona unaweza usimpeke na ukajipigia kitalebani kwani kipi kinashindikana sasa sikilizia nitakavyopita naye huyu mototo

Mwenetu iyo itakua kesho kama tutauona uzima ngoja nirudi mzigoni nikakuletee vitu vya kutosha mwenetu wa ukweli mwenyewe.


0 comments:

Popular Posts