NA MWANA KIJIWE
Habari za saa hizi mwenetu mwenyewe hopu umeamka gui kabia mi mwanao mbona niko okey kama Kenya yani sina mushikeli na mtu. Ila kama mwanangu leo diaini mambo yana kuzingua pole sana ila ndio ukuaji huo mwenetu komaa tu utatusua.Hivi wewe ulishawahi kusikia hizi ishu za watoto wa kike mavyuoni kujifotoa mapicha na kuyaweka insta kama siyo kurushiana na mabwana zao watspp? ekhee!! hizo hizo sasa juzi si kimenuka maeneo Fulani hapa town unaambiwa bi mwenye hausi kawaka mbaya
Kisa ni hizi smati foni ujue ni nzuri ila zina majanga yake mwenetu sasa unaambiwa faza mwenye hausi dizaini aliamua kuanya maadhimisho a ujana akaona isiwe shazi akavuta kitu yake toka chuo kimoja hapa town akawa anachepuka kishikaji ujue ndio maana kitaa chetu sisi tunapita na douta zao yani.
Basi unaambiwa kuchepuka chepuka si mtoto akawa anamtumia mapicha yale ya ndaniujue mzee alikuwa kadata na toto lle fulu kunawiri na maujuzi si ndio leo msalawaifee anachezea chezea foni ya mzee ikaingia sms watsApp image kwanza b mwenye hausi akaipotezea akaona dizaini haimuusu afu siyo mpango kwani anamweshimu mumewe akavunga akiendelea na mambo yake
Mara sms ya pili tena namba ile ile akavunga ya tatu nayo akavunga ila hii ya nne akachezwa kama na chale flani hivi ujue hi ilikuwa ni sms ya maneno siyo picha tena "nimekutumia zile za juzi hotel" ila bi mwenye hausi mwelewa kweli yani akaona haimhusu ki vile ngoja atulie labda atakuja kuuliza badae ghafla ikainga "bby zile za jan nazo umeziona?, mbona hata unisifii shape jaman lv?" Aah!! hapo unaambiwa bi mwenye hausi mapigo ya moyo juu huku anatetemeka tu si ndio akazifungua zile picha!, mzee hapo yupo na mambo zake home library si unajua vigogo tena.
Yani alisikia kilio tu toka chumbani unaambiwa michepuko noma mshikaji wangu baki njia
0 comments:
Post a Comment