background img

The New Stuff

UNAAMBIWA DAMBWENI, TEBO TEBONI WANA TUNAKAMUA MAJIPU!




Na Zee Trojani
Adje adje watu wangu wa ukwe ee!!! Ee! Si kweli wewe ni mtu wangu wa ukweli watoto wa kishua wanamwitaga besti frendi! Sasa Yule besti frendi wangu ndio wewe mwanangu mwenyewe, ujue kuchukua muda wako na kunisoma mwanao ni bonge ya shavu? Ni vile tu sipo karibu nikupe madala kadhaa mwanangu wa ukwe ee!! Yani ili jina mwanangu wa ukwe ee!! Si unajua vile tunalitamkaga pale kijiweni … ekhee!! Hivyo hivyo wala ujakosea si ndio maana nikasema wewe ndio mchizi wangu yani  ndio vile vile umepatia mwenetu mwenyewe mashavu sana yani wenye miji yao wanasemaga barida barafu hahah!!! Ujue watoto wa Arachuga na pale Mo Town huwa wananifurahishaga sana wao waasema baridi ya Yesu! Awa jamaa ni ma masi nondo si unajua Ibada ibadani kulaleki ujue na wewe mwanangu ili zile mishe ziweze kwenda kwenye reli saa Godi lazima umuweke mbele mbeleni yani au siyo mwenetu? Kula tano kwanza maana wewe ndio Yule mchizi wangu ninae mkubaligi.

Asa tuachane na hayo yote tudondoke mzigoni asa kule penyewe nilipokutolea madini mi mwanao si unanijua ni fulu apolo asa mgodi ndio kile kijiwe chetu wenyewe wanakiitaga dambwe! Unajua dambwe wewe?..sasa kwanini usilijue kwa mfano wakati wwe ndio Yule mchizi wangu wa ukwe ee!!. Asa pale dambweni leo ndio nilikuwa pale mchana flani wenye baridi la Yesu, si unakumbuka zile za kukimbizana na mzee wa majipu? Asa wana hatulalai yani ni fulu macho kodo na kila cha nyuzi si unajua kila cha nyuzi ni kitu gani? Aaaah!! Mwenetu ni magazeti si unaona yanatuangushia mzigo kila siku mara pale katumbuliwa kigogo mara kule napo ni jipu hahah ni fulu kutumbuana sikuizi hadi wana nao wananitumbua na mimi eti jipu! Hahah kwani mi mwenetu ni jipu? Kwanza kivipi yani, alafu unaanzaje kunifanya Zee jipu?

Sasa kweny e kile cha nyuzi kuna jipu wana wamelizogoshea mitikasi kibao yani Ooh! Sasa sisi tutafanya vipi michongo yetu Ooh!! Sisi puli tebo ndio ajira yetu, si umeshanisoma mwenetu sasa ujue huku dambweni wana wanatengeneza mipesa kibao yani kama angepita JPM basi uku ni jipu flani limejificha, Okhooo!! Wenetu kwani nimewachoma? Ila hakuna aliyesikia huku tupo na wana tu wale TRA huku hawapitagi si unajua zao ni ze gadiani ma deile nyuzi wenyewe wananyuzika kizungu tu ila ene wei kwa leo tusiwa maindi maana ujue nao wanazingua kinoma yani kutopupa mashavu ila no sweti au sio masela? Leo tuchezeshe za dambweni tu, asa Zee ndio nakuwa adicoketi wetu kwa mfano si unajua mwenenu nikila suti zao za italia aaah! Mbona kingereza kinakuja chenyewe tu alafu nikianza agiyu huko kwa wakubwa ni fulu maruhusa tu dambweni, msikonde wala nini mwenenu nipo gado tu mbona.

Asa kwa mfano pale kwa Shomari mfupi unazani tunapoteza madola mangapi kwa saa?  Mwanao mtu mzima ujue mpaka ana kompleini masela wanalisha viji pale kwa kuzungusha tebo tu! Ujue pale tunalipiaga cha samunge si unakijua mwanetu jero si pesa ndogo mpaka imewekwa ya silva. Ila badae masela nitawaibukia tufanye madoido kwa mzee wa majipu kama vipi ngoja nizingushe tebo ujue tebo inatembea na chupa ya laga flani, sas huku hizo hatuna tuna nyonya tu cha mchawi si unakijua wewe mwenetu ntakikuletea yani ukikipiga tu lazima ugande kwanza kisoja theni mishe ziendelee, ila itabidi upige misoso mwenetu kabla ujapiga cha mchawi maana vifafa kwa dambwe kesi yakujisevu mwenyewe wana wana chinja kona huku.

0 comments:

Popular Posts