background img

The New Stuff

FULL LOVE KITAA STORY, NI KAMA ZALI AU NOUMA TROJAN MAUJANJA NDANI YA MTEGO WA JIMAMA MATATAAAA!!



Na Trojan Maujanja.

Kwani na wewe mwanangu bado hujapata jidude bwaku bwaku la kwenye 6 by 6? Aaah!! acha kuniangusha mwanao kwama bado hujafanya mautundu ukashika mdude wa kwako na bosi flani pande za ushuani.

ene wei leo basi ngoja nikupe mchongo atari atari si unajua mimi mwanao Trojani Maujanja siishiwagi sera yani wewe ukitaka maujanja ya namna za kusanuka hapa tauni basi tusomane mwenyewe ndio ushindwe tu! si ndiyo nipeni dili maselaa!!? sasa mimi ndio nakutonya leo mwenetu.

Ila usi maindi sana maana siyo ishu wala nini basi leo mwanao natoka zangu kitaa si uajua kitaa ndio ofisi mwenetu unaambiwa ile nimepiga hatua kadhaa tu ndinga ilo shwaaaaa!!! limepozi miguuni si unanijua mwanao sinaga papara kwanza ile kucheki ndula kama imechafuka ki slomosheni si unajua zile za ndi ndi ngii!!

ndula bado safi afu ndio nikaangalia kioo kilichokuwa kinashuka taratiibu ebwanaa ee unaambiwa ni lile  toto princesss la geti flani kama gontanamo! kwanza nikahisi vipi huyu leo kakosea njia nini au anataka nituma nimpitishie mzigo mpya bdae nini...wewe kausha mwenetu sikiliza tori tu hili kuhusu mzigo mpya wewe usiulize uwo siku nyingine au siyo? kula tano kwanza.

sasa unaabiwa Trojan Mtukutu maujanja nikamwita kwanza "Aaah!! princesss!! dada la dada kulikoni na izi shrwaraa!! miguuni kwangu kwema lakini?" sasa kwanini mtoto asicheke japo kanitembea umri kama 37 hivi ila hapa si ndio kwa Trojan au? A.K.A Ticha wao? basi kuwa mpole.

toto likanipa jibu simpo tu, "nilitaka nikugonge wewe" hulu tabasamu likizidi si ndiyo ile welcome fest deti au siyo hahah mwana anacheeka. Trojan hizo nishazisomea kwa watoto kibao nikaona nirudishe majibu chaapu nikatabasamu. "vipi unaenda wapi Trojan?"  toto likaendelea kiasali asali "nipo kitaa tu nanyoosha nyoosha miguu bibiye" madoido hayo nikayaongeza si unajua mazombi ni vitendo lugha hakuna kabisa au siyo mwenetu? ndio maana nakukubaligi sana wewe.

"Basi naomba nisindikize Moli Mlimani" mtoto huyo akazidi tiririka tu, sasa kwanini agome kufunguka?, " kuna ombi lako ambalo naweza kataa kweli bibiye? labda kukumisi tu kimwali" unaambiwa hawa dada zetu wanapenda makonfidensi na mimi kwani nachelewaga basi huyo fastaa nshafungua mlango na kujitupia nani kama vile ndinga langu kulalekii, mtoto ni kucheka tu! si unajua hapendi uza sura kitaa pale ni tinted tu!.

"Ako kagauni kamekubamba wewe mtoto kama umezaliwa nacho vile, au ni cha special oda nini?" mtu mzima nikafungukia kigauni si unajua komplimenti muhimu kwa dada zetu, wewe sifia tu utaona mwenyewe mtoto atajaa chwaa!! alafu unamchota tu! au siyo? kula tano mwenetu!. haoo hadi Moli pale mtu mzima nikaona isiwe kesi ngoja nijivike upapaa leo mtoto ni kumfurahisha tu na katrey kake..sasa kwanini makonfidensi yasitawale uwanja?

mtoto kapiga shoppini zake pale kachanja kadi stori imeisha sasa tunarudi kitaa, hapo ndio mtu mzima mawazo yakahama resi sana hadi maili elfu nyingi sana si unajua pale unauona mzigo huo alafu gafla unahisi utapotea vile, sasa mwanao nikaanza panga mahesabu mengi "Trojan leo nakupeleka hadi kwangu huku hushuki leo, hahah!!" iyo ndio kauli ilinirudisha dunia mwanao nikamgeukia mtoto ni fulu kujichekesha na weupe wake wa chungwa ajajua tu mwanao ni zaidi ya mdigo navyomenya ayo machungwa

Itaendelea...


0 comments:

Popular Posts